METDO Tanzania

METDO Tanzania

Sunday, October 1, 2017

Awamu ya pili ujenzi wa reli Standard Gauge kuanza Oktoba

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli (RAHCO), Masanja Kadogosa akibadilishana mkataba na Makamu Mwenyekiti wa Kampuni ya Yapi Merkezi, Erdem Arioglu (kushoto) anayeshuhudia katikati ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa na Kaimu Balozi wa Uturuki nchini, Nevzat Arslan (Picha na Katuma Masamba

Serikali imesaini mkataba na kampuni ya Yapi Merkezi kwa ajili ya ujenzi wa awamu ya pili ya Reli ya Kisasa ya Standard Gauge (SGR) kutoka Morogoro hadi Makutupora mkoani Dodoma baada ya ujenzi wa awamu ya kwanza kuanza Aprili, mwaka huu.

Hafla ya utiaji saini umefanyika leo (Ijumaa) katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) ikishihudiwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa ikimuhusisha Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli (RAHCO), Masanja Kadogosa na Makamu Mwenyekiti wa Kampuni ya Yapi Merkezi, Erdem Arioglu.

Akizungumza kabla ya kusaini mikataba hiyo, Waziri Mbarawa amesema, reli hiyo itakuwa chachu ya maendeleo kwani itachangia kushuka kwa gharama za bidhaa na hivyo kuleta unafuu wa maisha kwa watanzania.

“Watu wengi wanafikiri reli inajengwa siku moja, ujenzi wa reli unachukua muda mrefu na una hatua tano…serikali imedhamiria kuhakikisha reli ya kati inajengwa kwa kiwango cha Standard Gauge,” amesema Mbarawa.

Aidha, ameongeza kuwa serikali inaendelea kutafuta vyanzo vya fedha zaidi na mikopo nafuu isiyo na masharti magumu ili kuhakikisha mradi huo unajengwa. Jiwe la msingi la ujenzi wa awamu ya pili ya reli hiyo litawekwa mwishoni mwa mwezi ujao.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com