Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akihutubia wakati wa ufunguzi wa
Semina ya siku moja ya wadau wa sekta ya ujenzi iliyohusu uboreshaji wa
utendaji kazi wa Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC), jijini Dar es Salaam
jana.
Mwenyekiti wa Baraza hilo Mayunga
Nkunya (wa tatu kushoto) akimpongeza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa baada ya kutoa hutuba yake.
Mwenyekiti wa Baraza hilo Mayunga Nkunya, akitoa hutuba katika semina hiyo.
Wadau wa sekta ya ujenzi wakiwa kwenye semina hiyo wakimsikiliza Wziri Mbarawa.
Wadau wa sekta ya ujenzi.
Taswira ya ukumbi wa semina.
Wadau wa sekta ya ujenzi wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi Waziri Mbarawa.
Na Dotto Mwaibale
WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ameliagiza Baraza la Taifa la
Ujenzi (NCC) kuhakikisha linaanisha gharama za Ujenzi wa miradi
mbalimbali badala ya kutegemea makadilio ya Wakandarasi wanaopetekeleza
miradi.
Alisema hayo Jijini Dar es salaam jana
wakati akifungua Semina ya Wadau wa Ujenzi iliyoandaliwa na Baraza la
Taifa la Ujenzi ambapo amesema kutokan na utaratibu mbovu uliopo hivi
sasa Watanzania wanatumia hata vifaa visivyokuwa na ubora wowote.
“Sekta ya ujenzi ina mchango mkubwa
katika kukuza pato la taifa na huwezesha utekelezaji wa miundombinu
mbalimbali kuimarika na kuwa kichocheo kikubwa kwa sekta nyingine za
kiuchumi ikiwe kilimo,utalii nishati na viwanda” alisema Mbarawa.
Mwenyekiti wa Baraza hilo Mayunga Nkunya
amemhakikishia Waziri huyo kuwa changamoto zote zilizopo kwenye Sekta
hiyo zitajadiliwa katika Semina hiyo na kupatiwa majibu ili kuepusha
hasara na athari ambazo zinaweza kulikumba Taifa endapo hatua
hazitachukuliwa.
Alisema changamoto ambazo waziri amewapa
amezitoa kwa baraza watazisimamia vizuri na kuhakikisha viwango vya
ujenzi vinatekelezeka kwa lengo la kuimarisha ubora wa majengo na
miundombinu kwa ujumla.
Aliongeza kuwa kutokana na kukosekana
kwa Ushirikiano kutoka kwa wadau wa Ujenzi ndio sababu za changamoto
hizo kujitokeza hivyo kupitia mkutano huo anaamini watafungua sura mpya
ya maendeleo katika sekta hiyo na taifa kwa ujumla.
0 comments:
Post a Comment