Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo akizungumza na viongozi mbalimbali wa serikali.
Majengo mapya yaliyokarabatiwa katika shule ya msingi Ihembe.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo akiwa na viongozi wa Kagera.
Baadhi ya wananchi wa Ihembe wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo kwenye uzinduzi wa madarasa yaliyokarabatiwa.
Wananchi wa kijiji cha Ihembe wilayani Karagwe Mkoani Kagera wameishukuru serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kukarabati miundombinu ya shule yao msingi ya Ihembe ambayo hapo awali ilikuwa katika hali mbaya.
Awali wanafunzi wa shule hiyo walikuwa wakisomea katika madarasa machakavu sana ambayo yalijengwa tangu mwaka 1948.
Kufuatia hali hiyo, Julai mwaka jana Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo alifanya ziara shuleni hapo na kukutana na hali hiyo ambayo ilimhuzunisha na kuamua kutafuta fedha kwa ajili ya ukarabati wa shule hiyo.
Kwasasa shule hiyo ina vyumba vitano vya madarasa, matundu ya vyoo nane, pamoja na stoo zimeboreshwa kisasa.
Katika uzinduzi huo, Waziri Jafo amempongeza Mbunge wa Jimbo la Karagwe Innocent Bashungwa kwa ushirikiano mkubwa anaoufanya katika Ofisi ya Rais TAMISEMI hadi kufanikiwa utekelezaji wa mradi huo pamoja na miradi mingine ya Afya, na barabara.
Jafo anaendelea na ziara yake mkoani Kagera ya uzinduzi wa miradi pamoja na kutembelea miradi mbalimbali akiwa na Kamati ya Bunge ya Utawala na TAMISEMI.
0 comments:
Post a Comment