Mwenyekiti wa Kituo cha Usuluhishi wa
masuala ya kijamii na kijinsia, CRC, Saida Mukhi akizungumza na
washiriki wa warsha kwa wadau wa utoaji wa huduma za msaada wa kisheria
na ushauri nasihi kwa wahanga wa vitendo vya ukatili wa kijinsia kwenye
wilaya mbili za mkoa wa Dar es Salaam, Kinondoni na Ubungo. Kulia ni
Mratibu wa Kituo cha Usuluhishi cha CRC, Bi. Gladness Munuo.
Mwenyekiti wa Kituo cha Usuluhishi wa
masuala ya kijamii na kijinsia, CRC, Saida Mukhi (kulia) akizungumza na
washiriki wa warsha kwa wadau wa utoaji wa huduma za msaada wa kisheria
na ushauri nasihi kwa wahanga wa vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Ofisa Mradi wa Kituo cha Usuluhishi wa
masuala ya kijamii na kijinsia, CRC, Suzan Charles akitoa ufafanua juu
ya mradi wa utoaji wa huduma za msaada wa kisheria na ushauri nasihi kwa
wahanga wa vitendo vya ukatili wa kijinsia kwenye wilaya mbili za mkoa
wa Dar es Salaam.
Mmoja wa washiriki wa warsha hiyo kwa wadau wa utoaji wa huduma za msaada wa kisheria na ushauri nasihi akichangia mada.
…………………………………………………………………..
KITUO cha Usuluhishi wa masuala ya
kijamii na kijinsia, CRC kimezinduwa mradi wa utoaji wa huduma za msaada
wa kisheria na ushauri nasihi kwa wahanga wa vitendo vya ukatili wa
kijinsia kwenye wilaya mbili za mkoa wa Dar es Salaam, yaani Kinondoni
na Ubungo.
Akizungumza na wadau wa mradi huo yaani
baadhi ya wasaidizi wa sheria, maofisa ustawi wa jamii, wanasheria,
mahakimu, Askari Polisi Dawati la Jinsia, maofisa watendaji wa mitaa
kutoka wilaya za Kinondoni na Ubungo, Mwenyekiti wa CRC, Saida Mukhi
aliwataka wadau hao kushirikiana ili kuhakikisha vitendo vya ukatili wa
kijinsia vinakomeshwa na kupungua.
Alisema lengo la mradi huo unaofadhiliwa
na shirika la Legal Service Facilities (LSF) ni kuhimarisha zaidi
upatikanaji wa msaada wa kisheria na ushauri nasihi kwa wahanga wa
ukatili wa kijinsia. Aliongeza kuwa mradi huo utajikita zaidi katika
utoaji wa msaada wa kisheria na ushauri nasihi kwa waathirika na
kuhakikisha mfumo wa upatikanaji wa haki unafanya kazi vizuri.
“…wadau katika maeneo hayo mnatakiwa
kuhakikisha tunapinga vitendo vya ukatili wa kijinsia ambavyo vinaweza
kusababisha madhara ya mwili, kingono au kisaikolojia au mateso kwa
wanajamii, ikiwa ni pamoja na wahusika kunyimwa uhuru,” alisema Bi.
Saida Mukhi akifungua warsha ya wadau hao.
Kwa upande wake, Mratibu wa Kituo cha
Usuluhishi cha CRC, Bi. Gladness Munuo akifafanua zaidi kwa washiriki wa
semina hiyo alisema mradi huo utaendeshwa katika Kata za Makumbusho na
Kawe kwa Wilaya ya Kinondoni huku kwa Wilaya ya Ubungo utajikita kwenye
Kata ya Saranga.
Alisema CRC itashirikiana na wadau
katika maeneo hayo kuhakikisha inapiga vita vitendo vya ukatili wa
kijinsia ambavyo mara nyingi vimekuwa na madhara ya mwili, kingono au
kisaikolojia au mateso kwa wanajamii na mara nyingine kuwanyima uhuru.
Sehemu ya washiriki wa warsha kwa wadau
wa utoaji wa huduma za msaada wa kisheria na ushauri nasihi kwa wahanga
wa vitendo vya ukatili wa kijinsia kwenye wilaya mbili za mkoa wa Dar es
Salaam, Kinondoni (Kata za Makumbusho na Kawe) na Ubungo (Kata ya
Saranga).
Sehemu ya washiriki wa warsha kwa wadau
wa utoaji wa huduma za msaada wa kisheria na ushauri nasihi kwa wahanga
wa vitendo vya ukatili wa kijinsia kwenye wilaya mbili za mkoa wa Dar es
Salaam, Kinondoni (Kata za Makumbusho na Kawe) na Ubungo (Kata ya
Saranga).
Picha ya pamoja ya washiriki wa warsha
kwa wadau wa utoaji wa huduma za msaada wa kisheria na ushauri nasihi
kwa wahanga wa vitendo vya ukatili wa kijinsia wakiwa na mgeni rasmi Bi.
Saida Mukhi.
0 comments:
Post a Comment