METDO Tanzania

METDO Tanzania

Wednesday, October 26, 2016

OMOG:TUMEKUJA SHINYANGA KUCHUKUA POINTI 6, LENGO LA WANA SIMBA NIKUCHUKUA UBINGWA WA LIGI KUU


Na Alex Mathias,Dar es salaam

Timu ya Simba ya jijini Dar es salaam tayari imeshatua mkoani Shinyanga kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya Mwadui FC unaotarajiwa kuchezwa mwisho mwa wiki hii huku Kocha Mkuu Joseph Omog akitamba kuwa wamekuja kuchukua alama tatu muhimu.

Akizungumza baada ya kutua Shinyanga Omog,amesema kuwa nia yetu ni kuendelea kupata matokeo mazuri kwa kila mechi tunayokutana nayo na sio kwamba tunadharau wapinzani ila msimu huu tumejiandaa kutwaa ubingwa mapema na hiyo ndio kiu ya wanasimba.

“Tumekuja kupambana na kuondoka na alama zote kwa sababu tuna mechi mbili dhidi ya Mwadui FC na Stand United hivyo hatukuja kutalii na tunajua michezo yote itakuwa migumu kwetu ila wachezaji wangu wapo kwa ajili ya kupata ushindi”alisema Omog

Kwa sasa Simba ndio timu pekee ambayo imecheza mechi kumi na moja bila kupoteza hata mchezo mmoja na kujikusanyia alama 29 na kuwa kinara wa Ligi huku wachezaji wakiwa na morali na kiu ya kuchukua ubingwa msimu huu na wanaonekana kuwa na uchu wa mafanikio.

Ukiangalia kila idara msimu huu imekamilika na mchezaji yoyote anayeingia anaenda kufanya kazi yake ipasavyo na kumekuwa na wafugaji wengi pindi wanapopata nafasi ya kutupia na kwa sasa wafungaji vinara katika timu hiyo ni Shiza Kichuya na Mzamiru Yassin ambaye ameibuka ghafla na kuwa mwiba mkali kwa magolikipa ambapo kila mechi anacheka na nyavu tu.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com