METDO Tanzania

METDO Tanzania

Monday, September 4, 2017

WAFUGAJI WA NG’OMBE WA MAZIWA CHAKECHAKE PEMBA HAWAJUI NJIA YA KUFIKIA MAFANIKIO KATIKA UFUGAJI

 index
Na Masanja Mabula -Pemba
 
BAADHI ya wafugaji wa Ng’ombe wa maziwa shehia ya Vitongoji wilaya ya Chakechake kisiwani Pemba, wamesema hawajui njia ya kupita, ili kufikia maendeleo ya ufugaji kama wenzao walivyo katika shehia nyengine .
 
Walisema wamekuwa wakiwashuhudiwa wenzao wakipewa misaada, elimu, kuitwa mjini kuhudhuria mafunzo na kutembelewa ingawa wao bado hawajui njia wenzao waliopita hadi kufikia hatrua hiyo.

Wakizungumza na waandishi wa habari, wafugaji hao waliojikusanya kundi la watu watatu wakiwa na Ng’ombe zaidi ya wanne, walisema na wao wanatamani kufikia maendeleo lakini hawajui chochcoro ya kupita.

Walisema wanapowafuatilia wenzao hawawapi ukweli wa mambo, na huwaeleza kwamba wasubiri na wajikusanye pamoja, ingawa wao wanaendelea kula raha kupitia sekta ya ufugaji.

Kiongozi wa muda wa wafugaji hao Abdalla Khamis Abdalla, alisema Ng’ombe wao aliezaa hivi karibuni amekumbwa na ungojiwa wakuvimba kiwele na hawajui wapi wampate daktari.

Kiongozi huyo, aliasema wanapotafuta ushauri kwa wenzao hukosa ushirikiano wa kweli, jambo ambalo kinawarejesha nyuma katika kufikia maendeleo.

“Mwandishi sijui wapi panaposajiliwa vikundu vya ufugaji, hata sheha hajatwambia juu ya hili, na hawa wafugaji wenzetu wanaopata ufadhili hata wa kupewa dawa, wamekuwa wazito kutuelekeza, labda wewe mwa ndishi utusaidie”,alifafanua.

Hata hivyo wafugaji hao wamekubali ushauri wa waandishi wa habari, kwamba waachane ne kuwafuata wafugaji wenzao, na badala yake kumfika sheha wa shehia yao, ili kupata utaratibu.

Naye Salim Ali Said, alisema wamekijikusanya tu pamoja, lakini hawajajua nini wafanye, maana hawana muongozo wowote wa namna ya kufuga na kutafuta soko.

“Kwa sasa tunakamua maziwa Ng’ombe wawili, lakini maziwa tunayageya kwa shilingi kati ya 800 au shilingi 900 kwa lita moja, lakini tutafuata ushauri wenu kwenye kwa sheha”,alifafanua.

Mwenyekiti wa kikundi cha ‘Tumaini’ kinachojishughulisha  pia na ufugaji, Mohamed Abdalla Khamis ‘song’ alisema wafugaji hao wamekuwa wazito kufuata taratibu kama tunavyowaelekeza.

“Sisi hawa ni jirani zetu, lakini wao na wengine wanadhani mkiunda kikundi tu siku ya pili, ndio maendeleo yanamiminika, sasa ni wazito au hawajafahamu nini maana ya kujitolea”,alieleza.

Sheha wa shehia ya Vitongoji wilaya ya Chakechake Ayoub Salim Suleiman, aliwataka wafugaji hao kumfika mara moja, ili kuwapa barua ya uthibitisho na kufuatilia taratibu za uanzishwaji wa kikundi cha ufugaji.

“Mimi hapa ofisini kwangu sisajili kikundi kiwe cha wafugaji, mboga, hisa au michezo lakini wananchi wakishajikusanya basi waje haraka niwaelekeze”,alifafanua.

Katika hatua  yengine Sheha huyo, alisema maendeleo ya mtu mmoja mmoja, ni vigumu kufikia na nia inayotumiwa sasa na wananchi ni kujikusanya pamoja.

Hata hivyo baadhi ya wananchi walioamua kujikusanya pamoja kwa shughuli mbali mbali kama za kilimo, ufugaji na kuweka na kukopa, walisema tatizo linalowakumba waliowengi ni kukosa umadhubuti.

Maryam Saleh Juma Mwenyekiti wa kikundi cha Hisa cha ‘wema haozi’ alisema kama hakuna kuaminiana na umakini wa hali ya juu, vikundi kadhaa vitanzishwa bila ya kufikia lengo.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com