Na Masanja Mabula -Pemba
BAADHI
ya wafugaji wa Ng’ombe wa maziwa shehia ya Vitongoji wilaya ya
Chakechake kisiwani Pemba, wamesema hawajui njia ya kupita, ili kufikia
maendeleo ya ufugaji kama wenzao walivyo katika shehia nyengine .
Walisema
wamekuwa wakiwashuhudiwa wenzao wakipewa misaada, elimu, kuitwa mjini
kuhudhuria mafunzo na kutembelewa ingawa wao bado hawajui njia wenzao
waliopita hadi kufikia hatrua hiyo.
Wakizungumza
na waandishi wa habari, wafugaji hao waliojikusanya kundi la watu
watatu wakiwa na Ng’ombe zaidi ya wanne, walisema na wao wanatamani
kufikia maendeleo lakini hawajui chochcoro ya kupita.
Walisema
wanapowafuatilia wenzao hawawapi ukweli wa mambo, na huwaeleza kwamba
wasubiri na wajikusanye pamoja, ingawa wao wanaendelea kula raha kupitia
sekta ya ufugaji.
Kiongozi
wa muda wa wafugaji hao Abdalla Khamis Abdalla, alisema Ng’ombe wao
aliezaa hivi karibuni amekumbwa na ungojiwa wakuvimba kiwele na hawajui
wapi wampate daktari.
Kiongozi
huyo, aliasema wanapotafuta ushauri kwa wenzao hukosa ushirikiano wa
kweli, jambo ambalo kinawarejesha nyuma katika kufikia maendeleo.
“Mwandishi
sijui wapi panaposajiliwa vikundu vya ufugaji, hata sheha hajatwambia
juu ya hili, na hawa wafugaji wenzetu wanaopata ufadhili hata wa kupewa
dawa, wamekuwa wazito kutuelekeza, labda wewe mwa ndishi
utusaidie”,alifafanua.
Hata
hivyo wafugaji hao wamekubali ushauri wa waandishi wa habari, kwamba
waachane ne kuwafuata wafugaji wenzao, na badala yake kumfika sheha wa
shehia yao, ili kupata utaratibu.
Naye
Salim Ali Said, alisema wamekijikusanya tu pamoja, lakini hawajajua
nini wafanye, maana hawana muongozo wowote wa namna ya kufuga na
kutafuta soko.
“Kwa
sasa tunakamua maziwa Ng’ombe wawili, lakini maziwa tunayageya kwa
shilingi kati ya 800 au shilingi 900 kwa lita moja, lakini tutafuata
ushauri wenu kwenye kwa sheha”,alifafanua.
Mwenyekiti
wa kikundi cha ‘Tumaini’ kinachojishughulisha pia na ufugaji, Mohamed
Abdalla Khamis ‘song’ alisema wafugaji hao wamekuwa wazito kufuata
taratibu kama tunavyowaelekeza.
“Sisi
hawa ni jirani zetu, lakini wao na wengine wanadhani mkiunda kikundi tu
siku ya pili, ndio maendeleo yanamiminika, sasa ni wazito au
hawajafahamu nini maana ya kujitolea”,alieleza.
Sheha
wa shehia ya Vitongoji wilaya ya Chakechake Ayoub Salim Suleiman,
aliwataka wafugaji hao kumfika mara moja, ili kuwapa barua ya
uthibitisho na kufuatilia taratibu za uanzishwaji wa kikundi cha
ufugaji.
“Mimi
hapa ofisini kwangu sisajili kikundi kiwe cha wafugaji, mboga, hisa au
michezo lakini wananchi wakishajikusanya basi waje haraka
niwaelekeze”,alifafanua.
Katika
hatua yengine Sheha huyo, alisema maendeleo ya mtu mmoja mmoja, ni
vigumu kufikia na nia inayotumiwa sasa na wananchi ni kujikusanya
pamoja.
Hata
hivyo baadhi ya wananchi walioamua kujikusanya pamoja kwa shughuli
mbali mbali kama za kilimo, ufugaji na kuweka na kukopa, walisema tatizo
linalowakumba waliowengi ni kukosa umadhubuti.
Maryam
Saleh Juma Mwenyekiti wa kikundi cha Hisa cha ‘wema haozi’ alisema kama
hakuna kuaminiana na umakini wa hali ya juu, vikundi kadhaa vitanzishwa
bila ya kufikia lengo.
No comments:
Post a Comment