METDO Tanzania

METDO Tanzania

Sunday, September 24, 2017

Rungwe yatoa uwanja wa Tandale kutumika kwa michezo

01
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Anastazia Wambura akikagua uwanja wa Machinga uliopo mjini Tukuyu ambao umebadilishwa matumizi na Halmashauri ya Rungwe kwa kukosa sifa w badala yake uwanja wa michezo sasa utakuwa unatumika ule wa Tandale mjini humo.
03
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Anastazia Wambura akiongea na wananchi na wanamichezo (hawapo pichani) waliokuwa wanashiriki Tamasha la Ngoma za Jadi linaloratibiwa na Taasisis ya Tulia Trust mjini Tukuyu
04
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Anastazia Wambura         (wa pili kushoto) na Naibu Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson wakibeba nyoka anyetumiwa kwa kucheza ngoma ya Bogobogobo kutoka Bujora Mwanza. (Picha na Eleuteri Mangi, WHUSM, Tukuyu)
………………………………………………………………………………
Na Eleuteri Mangi, Tukuyu, Mbeya

Halmashauri ya Rungwe imebadilisha matumizi ya uwanja wa zamani wa mpira wa miguu uliopo mjini Tukuyu unaojulikana kama machinga kuendelea kutumika kwa matumizi mengine kutokana na kukosa sifa za uwanja huo kukosa sifa.

Badala yake Halmashauri hiyo imetoa uwanja wa Tandale uliopo mjini Tukuyu kutumika kwa michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu na matamasha mbalimbali.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa wilaya ya Tukuyu Bw. Julius Chalya alipokuwa akitoa taarifa fupi ya shughuli za maendeleo katika wilaya hiyo kwa Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Anastazia Wambura alipokuwa katika ziara ya kikazi mkoani Mbeya.

“Uwanja wa mwanzo unaojulikana kama uwanja wa Machinga uliokuwa unatumika kwa michezo kwa sasa haufai kwa matumizi ya michezo kwa kukosa sifa, hivyo halmashauri imebadilisha matumizi yake ili uendelee kutumika kwa matumizi mengine ikiwemo kituo cha mabasi yanayotoa huduma katika halmashauri na bishashara nyingine” alisema Mkuu huyo wa Wilaya.

Akizungumzia kuhusu uamuzi wa halmashauri wa kubadilisha matumizi ya uwanja huo wakati wa kufunga Tamasha la pili la Ngoma za Asili linaloendeshwa na Taasisi ya Tulia Trust, Naibu Waziri Wambura amesema kuwa Serikali inaendelea kusisitiza halmashauri ziendelee kutenga maeneo yanayofaa kwa michezo kwa kutimiza vigezo vinavyotakiwa kwa ajili ya michezo.

Uwanja wa Tukuyu uliokuwa unatumika zamani kwa michezo umekosa vigezo vya kuendelea kutumika kama uwanja wa michezo kutokana na vipimo vyake kuonesha kuwa ni mdogo kwa kiwango cha halisi unatakiwa kuwa na urefu wa mita 68 na huo wa Tukuyu una mita 44.

Kuhusu kuendeleza kiwanja cha Tandale ambao umetolewa na halmashauri kwa ajili ya michezo, Naibu Waziri Wambura ameliagiza Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kupitia Katibu Mtendaji wake Mohamed Kiganja kushirikiana na halmashauri hiyo kwa kutoa ushauri wa kitaalamu kuendeleza uwanja huo ili wananchi wa Rungwe waweze kuutumia kuboresha afya zao kwa kufanya mazoezi pamoja kunufaika na fursa za kiuchumi wakati wa mashindano mbalilmbali yatakayofanyika uwanjani hapo.

Kupatikana kwa uwanja wa Tandale utnaotumika kwa sasa kwa michezo mbalimbali mjini Tukuyu kumepokelwa na kwa furaha na wananchi waliofurika viwanja hivyo wakati wa kuhitimisha Tamamsha la pili la Ngoma za Jadi linaloratibiwa na Taasisi ya Tulia Trust ambapo mwasisi wake Naibu Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameanza kampeni ya kuirudisha timu ya Tukuyu Stars kwa kuwahamasisha Wabunge wa mkoa wa Mbeya na wananchi kuiwezesha  timu hiyo kurudi Ligi Kuu ya Tanzania ya Vodacom. 
Share:

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © 2025 WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com