Timu
ya wataalam kutoka katika Taasisi ya kuendeleza kilimo Afrika (AGRA) imekutana
na viongozi wa wizara ya kilimo na wizara ya Viwanda na Biashara lengo likiwa
ni kuajadiliana namna ya kuongeza uzalishaji na tija katika mazao ya
kilimo pamoja na uongezaji wa thamani wa
mazao hayo.
Mkutano
huo ambao umehudhuriwa na Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent
Bashungwa, Naibu waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba na Naibu Waziri kilimo Mhe.
Hussein Bashe, pamoja na Rais wa AGRA Afrika Dkt. Agnes Kalibata umefanyika
tarehe 29.07.2019 katika ukumbi wa mikutano wa kilimo IV mjini Dodoma ambapo
wamekubaliana.
Kuimarisha
uzalishaji wa mazao manne ambayo,ni alizeti, mahindi, mpunga pamoja na maharage
ya soya ambayo yanahuitaji mkubwa katika soko.
Akizungumza
katika kikao kazi hicho Rais wa AGRA Dkt. Agnes Kalibata amesema kwamba Tanzania inaweza kuwa ghala la chakula afrika
endapo itaendea kuwekeza kikamilifu
katika sekta ya mbegu hapa nchini kwa kuwa wakulima wengi hawatumii mbegu bora
za kilimo.
Akizungumza
katika mkutano huo Dkt. Kalibata amesema
wakati umefika kuongeza uwekezaji katika sekta ya mbegu kwa kuimarisha
miundombinu ya umwagiliaji katika
mashamba ya mbegu ili ziweze kuzalishwa kwa uhakika na kuongeza tija kwa
wakulima.
Hata
hivyo ameshauri wizara ya kilimo kuandaa jukwaa maalum la wazalishaji wa mbegu
(Seed Platform) ambalo litasaidia kuongeza uhusiano baina ya wazalishaji wa
mbegu wa serikalini na wa sekta binafsi katika kusaidia ukuaji wa viwanda hapa
nchini.
"Tanzania
ina viashiria vingi vinavyoweza kusaidia ukuaji wa viwanda vya kilimo Kama
wataongeza kiasi cha uzalishaji mbegu, kuongeza idadi ya wauzaji pembejeo za
kilimo (Agro- Dealer), kuimarisha huduma za ugani kwa wakulima na kuongeza
usajili wa makampuni ya mbegu" Alisema Dkt. Kalibata
Aidha
mwenyekiti wa kikao hicho ambaye ni waziri wa viwanda na biashara Mhe. Innocent
Bashungwa amesema wamekubalina na AGRA Kuweka mikakati madhubuti ya kuendeleza mazao ya mafuta ili kupunguza
uagizaji wa bidhaa hiyo nje ya nchi.
Hata
hivyo Mhe. Bashungwa
amesisitiza kwamba AGRA isaidie katika kuongeza uzalishaji wa mbegu hapa
nchini ambapo uzalishaji huo utasaidia
kuongeza malighafi za viwanda hapa nchini.
Akitolea
mfano viwanda vya alizeti Mhe. Bashungwa amesema kwamba hapa nchini kuna viwanda vya kusindika
alizeti vipatavyo 29 lakini vyote vinazalisha chini ya asilimia 30 kwa kukosa
malighafi za viwandani.
Mhe.
Bashugwa aliendea kumfafanulia Rais wa AGRA Afrika kwamba nchi zinazoizunguka
tanzania zinauhitaji mkubwa wa mazao kama soya,mahindi,alizeti mpunga na Degu
hivyo kwa ushirikiano huo utasaidia sana katika upatikanaji wa soko kwa
wakulima wetu.
Akiongea
kwa niaba ya serika Naibu Waziri Mh. Mgumba amesema makubaliano hayo yamelenga
kuongeza tija na uzalishaji kwa wakulima na kuongeza ushindani katika soko kuwa na bei nzuri kwa wanunuzi.
Hata
hivyo Mhe. Mgumba ameeleza kwamba
wakuima wanatakiwa kulima kulingana na mahitaji ya soko na kutokana na makubaliano hayo kutasaidia
wakulima kupunguza gharama za uzalishaji
hivyo kusaidia kupungua bei za mazao
ikilinganishwa na hali ilivyo
sasa.
Aidha,
wamekubaliana kuimarisha sekta binafsi hususani katika uzalishaji wa mbegu, huduma za
ugani na kuijengea mazingira mazuri ili kuweza kuongeza uzalishaji , na kutoa
ajira kwa watanzania kwa kupunguza gharama za uwekezaji
Naye
Mh Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amesema wakulima wanakabiliwa na changamoto
kubwa ya kiwango kidogo cha uzalishaji
katika ekari na gharama kubwa ya uzalishaji hivyo kuwashauri AGRA kuangalia
namna ya kuwasaidia wakulima kupunguza gharama ya uzalishaji na kuongeza
kipato.
Kwa
upande mwingine Naibu waziri Bashe amewaomba AGRA kusaidia uzalishaji wa mbegu
hapa nchini, ili ziweze kupatikana kwa gharama ndogo na mkulima kupata matokeo chanya.
Katika
kuimarisha ufuatiliaji wa shughuli za kilimo wamekubaliana kuhusu fedha
zinazotoka kwa wafadhili zijulikane kila
zinapokwenda ili kuhakikisha lengo lilikusudiwa linafikia alisema Mhe.
Bashe
MWISHO
0 comments:
Post a Comment