Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Dodoma,
Sosthenes Kibwengo,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)
wakati akitoa taarifa juu ya watuhumiwa waliokamatwa wakitoa rushwa na
kupokea mkoani Dodoma.
……………………
Na.Alex Mathias,Dodoma
TAASISI ya kuzuia na kupambana na rushwa
nchini (TAKUKURU) mkoa wa Dodoma inatarajia kuwafikisha mahakamani watu
saba wanaotuhumiwa kujihusisha na vitendo vya kuomba na kupokea rushwa
kinyume na kifungu cha sheria namba 11 ya mwaka 2007.
Moja ya watuhumiwa waliokamatwa ni
mfanyabiashara Bahadur Hirji (68) mkazi wa mtaa wa Tembo Kata ya
madukani jijini Dodoma na mwanae Nahid Bahadur (33) mhasibu wa Victory
Bookshop kwa kosa la kuahidi kumpa Mkuu wa wilaya Patrobas Katambi sh
mil 1.2 ili asifuatilie mapungufu katika utekelezaji wa amri ya Baraza
la Ardhi na Nyumba la Wilaya ya Dodoma kukazia hukumu iliowasilishwa
kwake.
Akizungunza na waandishi wa habari
Ofisini kwake Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Dodoma Sosthenes Kibwengo alisema
baada ya TAKUKURU kupata taarifa ya watuhumiwa kutoa fedha hiyo ya
kishawishi kwa Mkuu wa wilaya walianza kuwafuatilia na kufanikiwa
kuwakamata Julai 27 katika hoteli ya Royal village iliopo Area D baada
ya mtuhumiwa Nahid kumkabidhi Mkuu wa wilaya rushwa hiyo.
Kibwengo amesema kuwa ukiacha watuhumiwa
hao pia wamemkamata Omary Mtauka ambae ni msaidizi wa mtendaji wa Kata
ya Makutupora iliopo jijini Dodoma baada ya kupokea rushwa ya sh
110,000 kutoka kwa Mzee Paulo Mawope (78) mkazi wa Chilungule Kata ya
Makutupora ili wamalize tuhuma dhidi ya kugombana na jirani zake
zilizowasilishwa na Mtendaji wa mtaa na badae ofisini kwake.
“Awali tulipokea taarifa kutoka kwa
mjukuu wake kwamba amepigiwa simu na mtendaji wa Kata ya Makutupora
uchunguzi watu uliweza kuthibitisha juu ya uwepo wa tukio hilo,na
mtuhumiwa kujifanya ni mtendaji wa Kata hiyo,” alisema Kibwengo.
Hata hivyo amesema kuwa TAKUKURU
inamshikilia Stanley Motambi(34) ambayo ni mtendaji wa Kijiji cha
Matumbulu kilichopo Kata hiyo kwa kosa la kuomba na kupokea rushwa ya sh
65,000kinyume na taratibu za kiutendaji kutoka kwa Wilfred Mtundu
ambaye alikuwa na shauri la mgigoro wa Ardhi mbele ya mtendaji wa kijiji
kama kishawishi ili askilize shauri hilo.
Kibwengo amesema kuwa baada ya kupata
taarifa hiyo walifanya uchunguzi na kuthibitisha mtuhumiwa hiyo alitenda
kosa hilo Junior tatu mwaka huu.
Amewataja watuhumiwa wengine waliokamatwa
na vitendo hivyo vya rushwa ni Venance Mayo (34) na Sultan Rusheke (33)
ambalo ni walimu wa sekondari ya viwandani iliopo jijini Dodoma ambalo
waliomba fedha hiyo ili wampatie cheti cha utambulisho wa kusoma shule
hiyo (leaving certificate).
Mtoa taarifa ambaye alikuwa Mwanafunzi wa
shule hiyo alihitaji cheti hiko kwa ajili ya kuomba kozi fupi katika
taasisi Moja ndipo akaenda shuleni hapo.
Amesema kuwa taarifa hiyo ikiwafikia
TAKUKURU Julai 26 na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa Mayo akiwa kwenye
Bajaji yenye namba MC686BHK ilioegeshwa kwenye uzio wa shule hiyo
baada ya kupokea hongo hiyo na kumkabidhi muhusika cheti huku akiwa na
muhuri wa Mkuu wa shule na kugonga kwenye cheti,kabla hajaondoka ndio
alikamatwa ikiwemo Rusheke pia kwa sababu amehusika kutoa.
Mtuhumiwa Mwingine aliyekamatwa na ni
Abdulhakim Kabunga (26) ambaye ni mtumushi wa muda wa mamlaka ya
vitambulisho nchini (NIDA) Dodoma ambayo alikamatwa Julai 27 baada ya
TAKUKURU kupata taarifa ya kwamba amepokea rushwa ya sh 30,000 kutoka
kwa mtu mmoja aliyekuwa akihitaji kitambulisho cha taifa ili amsaidie
kuipata haraka.
Hata hivyo amesema kuwa baada ya kuhojiwa
mtuhumiwa huyo amekiri kuhusika na kitendo hiko huku taasisi hiyo
ikiwakumbusha watu wanaofuatilia vitambulisho vya NIDA zoezi hilo
utilewa bure na iwapo watatakiwa kutoa rushwa ili wahudumiwe wanatakiwa
kutoa taarifa TAKUKURU.
Aidha Kibwengo,ameendelea kuwakumbusha
watumishi wa umma na wakazi wa Dodoma kwa ujumla kuzingatia maadiki ya
utumishi ili kujiepusha na vitendo hivyo kwani vinaminya haki za
wananchi.
0 comments:
Post a Comment