Katibu Mkuu Wizara ya Afya
,Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto (Wizara ya Afya) Dkt. Mpoki
Ulisubisya akiongea na wadau mbalimbali wa sekta ya Afya hawapo pichani
wakati wa uzinduzi wa mpango wa Taifa wa usimamizi wa Takwimu za Afya
uliofanyika jijini Dar es salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya
,Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto (Wizara ya Afya) Dkt. Mpoki
Ulisubisya katikati akiongoza wadau mbalimbali wa sekta ya ya afya
wakishikana mikono na kunyosha juu kuashiria kuzindua rasmi wa mpango
wa Taifa wa usimamizi wa Takwimu za Afya uliofanyika jijini Dar es
salaam.
Wadau mbalimbali wa sekta ya afya
wakishikina mikono kwa pamoja wakiongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya
,Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto (Wizara ya Afya) Dkt. Mpoki
Ulisubisya hayupo pichani kuashiria na kuzindua rasmi wa mpango wa
Taifa wa usimamizi wa Takwimu za Afya uliofanyika jijini Dar es salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya
,Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto (Wizara ya Afya) Dkt. Mpoki
Ulisubisya katikati waliokaa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya
Wadau mbalimbali wa sekta ya afya wakati wa uzinduzi wa mpango wa Taifa
wa usimamizi wa Takwimu za Afya uliofanyika jijini Dar es salaam.
Wadau mbalimbali wa sekta ya afya
wakifuatilia kwa makini hotuba ya Katibu Mkuu Wizara ya Afya ,Maendeleo
ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto (Wizara ya Afya) Dkt. Mpoki Ulisubisya
hayupo pichani wakati wa uzinduzi wa mpango wa Taifa wa usimamizi wa
Takwimu za Afya uliofanyika jijini Dar es salaam. Picha Na WAMJW.
…………………………
NA WAMJW-DAR ES SALAAM
MPANGO wa Taifa wa usimamizi wa
Takwimu za Afya umezinduliwa rasmi ili kuweka kumbukumbu sahihi za
taarifa za afya zinazosaidia katika kufanya tathimini, kupanga, na
kufanya maamuzi juu ya uboreshaji wa huduma za afya nchini.
Akiongea na wadau mbalimbali wa
afya jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi huo Katibu Mkuu Wizara ya
Afya Dkt. Mpoki Ulisubisya amesema kuwa Mpango huo utasaidia Serikali na
wadau mbalimbali wa sekta ya afya kufanya utekelezaji bora kutokana na
vipaumbele vilivyowekwa kupitia takwimu za nchi.
“Mpango huu utaiwezesha nchi
kulingana na mpango wa pamoja kwa kuweka vipaumbele ili kuwaleta pamoja
wadau wote wa maendeleo katika sekta ya afya nchini “ alisema Dkt.
Ulisubisya.
Aidha Dkt. Ulisubisya amesema kuwa
Tanzania imekuwa nchi ya tatu kusini mwa jangwa la sahara barani Afrika
kuzindua mpango huo ikitanguliwa na nchi jirani za Kenya na Malawi.
Mbali na hayo Dkt. Ulisubisya
amesema kuwa wanategemea pia nchi zilizoendelea, taasisi na Mashirika ya
kimataifa watakuwa tayari kuchangia mpango huo ili kuweza kufikia
malengo ya nchi waliyoweka.
0 comments:
Post a Comment