Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia baadhi ya vitu
vilivyotengenezwa na mikono wakati wa Ufunguzi wa Tamasha la Wasanii
Wanawake wa mkoa wa Kusini Unguja lililofanyika kwenye ukumbi wa Coco
Blue, Jambiani jana jioni. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Wasanii wa Kikundi cha Tausi
kutoka Kisiwandui wakitumbuiza wakati wa Ufunguzi wa Tamasha la Wasanii
Wanawake wa mkoa wa Kusini Unguja lililofanyika kwenye ukumbi wa Coco
Blue, Jambiani ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan. ( Picha na Ofisi ya
Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati kwenye
Ufunguzi wa Tamasha la Wasanii Wanawake wa mkoa wa Kusini Unguja
lililofanyika kwenye ukumbi wa Coco Blue, Jambiani jana jioni. (Picha na
Ofisi ya Makamu wa Rais)
Wasanii wa Kikundi cha Majalis
Saniya kutoka Michenzani wakitumbuiza wakati wa Ufunguzi wa Tamasha la
Wasanii Wanawake wa mkoa wa Kusini Unguja lililofanyika kwenye ukumbi wa
Coco Blue, Jambiani ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan. ( Picha na
Ofisi ya Makamu wa Rais)
Msanii
Sharifa Salum Hassan wa Kikundi cha Tausi kutoka Kisiwandui akionyesha
umahiri wa kucheza ngoma kwenye wa Ufunguzi wa Tamasha la Wasanii
Wanawake wa mkoa wa Kusini Unguja lililofanyika kwenye ukumbi wa Coco
Blue, Jambiani ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan. ( Picha na Ofisi ya
Makamu wa Rais)
……………………………………………………………..
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia
Suluhu Hassan jana alifungua Tamasha la Wasanii Wanawake wa mkoa wa
Kusini Unguja.
Tamasha hilo lililofanyika kwenye ukumbi wa Coco Blue
,Jambiani na kuhudhuriwa na Viongozi mbali mbali wa Chama na Serikali
pamoja na wananchi wa mkoa wa Kusini Unguja.
Makamu wa Rais aliwashukuru Waandaaji wa Tamasha hilo ambao wamesaidia kuwaleta wanawake wa mkoa wa Kusini pamoja.
Makamu wa Rais amewapongeza wanawake wa mkoa wa Kusini kwa
kuwa wa kwanza kutekeleza wazo lililowazwa na kuonyesha utamaduni wa
Kusini.
Mhe. Samia alisema Utamaduni wa zamani hauna budi kuendelezwa
ili vijana wa sasa wajue wapi tumetoka, wapi tulipo na wapi tunaelekea.
Akivitaja baadhi ya vitu alivyoviona kwenye ufunguzi huo kama
Manda, Mabobwe ,Vipopoo, ngoma ya Msanja ambavyo kwa pamoja vina lengo
la kuleta yale mazuri ya zamani ambayo yametutoka.
Alisema Vijana wengi hawajui Kiwe-jiwe la kusagia chakula
(Blender za Bibi zetu) wao wanajua Blender, hivyo ni vyema Tamasha hili
likaja na vitu vingi mwakani waelewe hata maji tuliyatunza kwenye
Mtungi ambao wao kwa sasa wanayajua Majokofu.
Hivyo aliwasihi Wanawake wa kusini kufufua tamaduni zetu na
kuzidumisha, alisema sema yeye anatoka Kizimkazi ambapo ngoma maarufu
ni Shomoo na Dandaro .
Makamu wa Rais alisema kuwa Utamaduni utasaidia kuwafunza
watoto wetu uzalendo,mazingira, nidhamu ya maisha kwani utamaduni
unajumuisha kila kitu kuanzia chakula, mavazi, vifaa
vilivyotumika,filamu, ngoma na burudani mbali mbali.
Mhe. Samia aliwapongeza sana wanawake wa mkoa wa Kusini kwa
kutoka kwenye utamaduni wa kukaa tu na badala yake kufanya shughuli
zinazowaingizia kipato. “Nimefurahishwa kuona wakina Mama sasa hivi
wanatoka wana Vikundi vya Kulima tumeonyeshwa wanalima Tungulee,
wanalima Karoti,wanalima michicha hii yote ni utamaduni kwamba tumetoka
kwenye utamaduni wa kukaa tu na kusubiri bwana haji lakini sasa tunatoka
tunajituma na sisi tunapata mapato yetu tunaendelea na maisha yetu”
Makamu wa Rais alisema ni wajibu wa kila mama kutunza na
kufundisha watoto wetu Tamaduni zetu, “Tunautamaduni ambao hautakiwi
kuonyeshwa mbele za watu na ule nao tufundishe watoto wetu, tusiuache ,
tunakuwa wa kisasa mno , tunajifanya wa kisasa mno kiasi ambacho mambo
mengine tunayaacha lakini ambao kwa sie tuliofanyiwa huko nyuma unajua
faida yake na watoto wetu wanaokosa kufanyiwa sasa hivi tunaona hasara
yake”
Mwisho Makamu wa Rais alitoa rai kwa waandaaji wa Tamasha
hilo kuhakikisha linafanyika kila mwaka na kujumuisha tamaduni mbali
mbali zenye lengo la kujenga na kuimarisha mshikamano pamoja na
kudumisha upendo na amani katika jamii, aliwashukuru wadhamini
waliosaidia kufanikisha Tamasha hilo.
0 comments:
Post a Comment