Sunday, September 3, 2017

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA TAMASHA LA WASANII WANAWAKE WA MKOA WA KUSINI UNGUJA

2
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia baadhi ya vitu vilivyotengenezwa na mikono wakati wa Ufunguzi wa Tamasha la Wasanii Wanawake wa mkoa wa Kusini Unguja lililofanyika kwenye ukumbi wa Coco Blue, Jambiani jana jioni. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
3
4 9
Wasanii wa Kikundi cha Tausi kutoka Kisiwandui wakitumbuiza wakati wa Ufunguzi wa Tamasha la Wasanii Wanawake wa mkoa wa Kusini Unguja lililofanyika kwenye ukumbi wa Coco Blue, Jambiani ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan. ( Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
17
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati kwenye Ufunguzi wa Tamasha la Wasanii Wanawake wa mkoa wa Kusini Unguja lililofanyika kwenye ukumbi wa Coco Blue, Jambiani jana jioni. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
22
Wasanii wa Kikundi cha Majalis Saniya kutoka Michenzani wakitumbuiza wakati wa Ufunguzi wa Tamasha la Wasanii Wanawake wa mkoa wa Kusini Unguja lililofanyika kwenye ukumbi wa Coco Blue, Jambiani ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan. ( Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
1 
23
Msanii Sharifa Salum Hassan wa Kikundi cha Tausi kutoka Kisiwandui akionyesha umahiri wa kucheza ngoma kwenye wa Ufunguzi wa Tamasha la Wasanii Wanawake wa mkoa wa Kusini Unguja lililofanyika kwenye ukumbi wa Coco Blue, Jambiani ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan. ( Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
……………………………………………………………..
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan jana alifungua Tamasha la Wasanii Wanawake wa mkoa wa Kusini Unguja.

Tamasha hilo lililofanyika kwenye ukumbi wa Coco Blue ,Jambiani na kuhudhuriwa na  Viongozi mbali mbali wa Chama na Serikali pamoja na wananchi wa mkoa wa Kusini Unguja.

Makamu wa Rais aliwashukuru Waandaaji wa Tamasha hilo ambao wamesaidia kuwaleta wanawake wa mkoa wa Kusini pamoja.

Makamu wa Rais amewapongeza wanawake wa mkoa wa Kusini kwa kuwa wa kwanza kutekeleza wazo lililowazwa na kuonyesha utamaduni wa Kusini.

Mhe. Samia alisema Utamaduni wa zamani hauna budi kuendelezwa ili vijana wa sasa wajue wapi tumetoka, wapi tulipo na wapi tunaelekea.

Akivitaja baadhi ya vitu alivyoviona kwenye ufunguzi huo kama Manda, Mabobwe ,Vipopoo, ngoma ya Msanja ambavyo kwa pamoja vina lengo la kuleta yale mazuri ya zamani ambayo yametutoka.

Alisema Vijana wengi hawajui Kiwe-jiwe la kusagia chakula (Blender za Bibi zetu)  wao wanajua Blender, hivyo ni vyema Tamasha hili likaja na vitu vingi mwakani waelewe hata maji tuliyatunza kwenye Mtungi ambao wao kwa sasa wanayajua Majokofu.

Hivyo aliwasihi Wanawake wa kusini kufufua tamaduni zetu na kuzidumisha, alisema  sema yeye anatoka Kizimkazi ambapo ngoma maarufu ni Shomoo na Dandaro .

Makamu wa Rais alisema kuwa Utamaduni utasaidia kuwafunza watoto wetu uzalendo,mazingira, nidhamu ya  maisha kwani utamaduni unajumuisha kila kitu kuanzia chakula, mavazi, vifaa vilivyotumika,filamu, ngoma na burudani mbali mbali.

Mhe. Samia aliwapongeza sana wanawake wa mkoa wa Kusini kwa kutoka kwenye utamaduni wa kukaa tu na badala yake kufanya shughuli zinazowaingizia kipato. “Nimefurahishwa kuona wakina Mama sasa hivi wanatoka wana Vikundi vya Kulima tumeonyeshwa wanalima Tungulee, wanalima Karoti,wanalima michicha hii yote ni utamaduni kwamba tumetoka kwenye utamaduni wa kukaa tu na kusubiri bwana haji lakini sasa tunatoka tunajituma na sisi tunapata mapato yetu tunaendelea na maisha yetu”

Makamu wa Rais alisema ni wajibu wa kila mama kutunza na kufundisha  watoto wetu Tamaduni zetu, “Tunautamaduni ambao hautakiwi kuonyeshwa mbele za watu na ule nao tufundishe watoto wetu, tusiuache , tunakuwa wa kisasa mno , tunajifanya wa kisasa mno kiasi ambacho mambo mengine tunayaacha lakini ambao kwa sie tuliofanyiwa huko nyuma unajua faida yake na watoto wetu wanaokosa kufanyiwa sasa hivi tunaona hasara yake”

Mwisho Makamu wa Rais alitoa rai kwa waandaaji wa Tamasha hilo kuhakikisha linafanyika kila mwaka na kujumuisha tamaduni mbali mbali zenye lengo la kujenga na kuimarisha mshikamano pamoja na kudumisha upendo na amani katika jamii, aliwashukuru wadhamini waliosaidia kufanikisha  Tamasha hilo.

No comments:

Post a Comment