METDO Tanzania

METDO Tanzania

Thursday, September 21, 2017

Kimbunga Maria chasababisha hasara kubwa Puerto Rico

media
Maafisa wa uokoaji katika mitaa ya Guayama, Puerto Rico, baada ya Kimbunga Maria, Septemba 20, 2017
Kimbunga Maria, kimesababisha uharibifu mkubwa katika eneo la West Indies. Kimbunga hiki kimeua watu saba katika kisiwa cha Dominica na kusababisha uharibifu mkubwa Puerto Rico.
Eneo hilo la Marekani liliharibiwa vibaya na kimbunga Maria siku ya Jumatano na upepo unaokwenda kilomita 250 kwa saa.
Kimbunga Maria kimekata umeme katika eneo lote la Puerto Rico, ambapo watu milioni 3.5 wanaishi katika kisiwa hiki.
Baada ya kimbunga Maria kupiga Puerto Rico, gavana ameamrisha watu kusalia manyumbani mwao kuanzia saa kumi na mbili jioni hadi saa kumi na mbili asubuhi.
Hi ni hatua ya kuwazuia watu kupata ajali kutokana na nyaya za umeme zilizoanguka na vifuzi vilivyo barabara za mji.
Kituo cha vimbunga cha Marekani kinasema kuwa mafuriko makubwa yanakikumba kisiwa hiki.
Kimbunga Maria kwa sasa kinaondoka katika kisiwa cha Puerto Rico na kimepunguza nguvu zake hadi kiwango cha pili, kwa mujibu wa wataalamu.
Mtazamo wa Satellite wa kimbunga Maria kwenye anga ya Puerto Rico, Septemba 20, 2017.

Wawili wapoteza maisha Guadeloupe

Kusini mwa Guadeloupe, eneo lililoathiriwa zaidi na kimbunga Maria siku moja kabla, watu wawili walipoteza maisha na wawili wamekosekana, kulingana na tathmini ya hivi karibuni. Katika kisiwa cha Marie Galante, ukanda wa pwani umeathirika zaidi. Baadhi ya barabara zimekubwa na mafuriko, na nyngine zimefunikwa na miti. Fukwe zimetoweka. Na kusini mwa mji wa Basse-Terre, familia 50,000 hazina umeme.

Baaba ya kuundwa kamati ya wahumbe kutoka wizara mbalimbali kwa ajili ya ujenzi wa Saint-Martin na Saint-Barthelemy, visiwa vinavyomilikiwa na Ufaransa vilivyoathirika zaidi na kimbunga Irma, Waziri Mkuu Edouard Philippe ametangaza kwamba tangazo la janga la asili litasainiwa siku ya Jumamosi Septemba 23 kwa Guadeloupe.

Watu saba wapoteza maisha katika kisiwa cha Dominica
Kisiwa jirani cha Dominicakimeathirika zaidi na Kimbunga Maria, pamoja na upepo unaokwenda kilomita 260 kwa saa.

"Tumepoteza kila kitu tulichokua nacho," Roosevelt Skerrit Waziri Mkuu wa Kisiwa hicho chenye watu 73,000, ameandika kwenye ukurasa wake wa Facebook.

Chanzo:RFI
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com