METDO Tanzania

METDO Tanzania

Thursday, September 21, 2017

Tetemeko lasababisha vifo vya zaidi ya watu 150 Mexico

media
Tetemeko la ardhi lenye nguvu ya 7.1 kwenye kipimo cha Richter lilmekumba Jumanne hii Septemba 19 nchi ya Mexico na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 150, kkulingana na idadi ya mwanzo iliyotolewa na maafisa wa serikali.

Tetemeko hilo limezua hali ya sintofahamu na watu kuwa na wasiwasi mkubwa katika nchi hiyo yenye wakazi milioni 20. Ni miaka 32 sasa tangu tetemeko jingine lenye nguvu lililoua zaidi ya watu 10,000 mwaka 1985.

Idadia ya watu waliopoteza maisha ni zaidi ya 150. Kwa mujibu wa kituo cha Marekani cha utabiri wa mambo ya tetemeko (US Geological Center USGS), kitovu cha tetemeko hiulo kilikua kimepatikana katika jimbo la Puebla, katika katikati mwa nchi, karibu na mji mkuu, kilomita 51 za kina.

Tetemeko hilo limedondosha karibu majengo 30 katika mji mkuu wa Mexico city.

Watu wanaotoa huduma za dharura wakisaidiwa na mamia ya watu wanaojitolea bado wanaendelea kutafuta manusura ambao wamefukiwa na kifusi.

Recibimos reportes de daños en edificios. Pedimos a la población seguir medidas de seguridad de @PC_Estatal. Continuamos revisión por #sismopic.twitter.com/Mw3LbHEH0P
  Tony Gali (@TonyGali) 19 septembre 2017
Maafisa wa serikali nchini wanasema idadi ya waliokufa inaweza kuongezeka.

Baadhi ya waandishi wa habari katika mji Mexico City wanasema kuna idadi kubwa ya watu waliofukiwa na kifusi baada ya majengo kuporomoka.

"Sijawahi kuona au kusikia tetemeko la ardhi lenye nguvu kama hili tangu nimeishi Mexico kwa miaka kumi na nane sasa. 

Nililisikia hata zaidi kuliko lile la Septemba 8 ambalo lilikuwa na ukubwa wa 8.2 kipimo cha Richeter, " amesema mwandishi wa rfi katika mji wa Mexico Ciy, Patrick John.

Chanzo:RFI
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com