METDO Tanzania

METDO Tanzania

Wednesday, January 26, 2022

MGODI WA SHANTA WAANZA KUTOA FURSA KWA WANASINGIDA

 



Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge wa tatu kutoka kushoto , akiwa na mkuu wa wilaya ya ikungi Jerry Muro na wafanyakazi wa  wa kampuni ya uchimbaji madini ya SHANTA GOLD alipofanya ziara kukagua miradi mbambali.

Wafanyakazi wa shanta gold wakiendelea na kazi , mkuu wa mkoa na akishuhudia kazi inavyofanyika .

Miongoni mwa madarasa ya shule ya msingi yaliyojengwa na shanta gold  ambayo mkuu wa mkoa dkt binilith mahenge aliikagua kwenye ziara yake.

Meneja mradi was hanta gold Kundael Mtiro akiwasilisha taarifa ya mradi kwa mkuu wa mkoa

Mkuu wa mkoa akizungumza wafanyakazi was hanta gold na wachimbaji  katika eneo mojawapo la uchimbaji wa dhahabu.

 

Mkuu wa mkoa wa singida Dkt. Binilith Mahenge  kushoto , Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ikungi Justice Kijazi katikati na Mkuu wa wilaya ya ikungi Jerry Muro wakizungumza wakati wa ziara kukagua miradi katika machimbo ya SHANTA GOLD  

 


Na Hamis Hussein – Singida

 

Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge  amewashauri wawekezaji mkoani hapa w kushirikiana na Halmashauri za Wilaya wakati wa kuanzisha miradi ya Maendeleo ya Kijamii (Community Socially Responsibility – CSR) ili kuwa na tija kweenye miradi hio na kuepuka matumizi makubwa ya fedha wakati wa utekelezaji wake.

Akizungmza na wafanyakazi wa machimbo ya madini ya dhahabu yanayochimbwa na kampuni ya Shanta Gold iliyopo kijiji cha Mang’onyi wilayani Ikungi alipofanya ziara kukagua mradi huo  Mkuu  huyo wa mkoa  Dkt. Mahenge mbapo alisema kuwa  miradi yote inayoanzishwa na wawekezaji ipitie katika Halmashauri za Wilaya ambazo zinafahamu mahitaji ya wahusika na  gharama halisi za ujenzi katika maeneo hayo.

Dkt. Mahenge alitolea  mfano kwa madarasa yalikamilika hivi karibuni kupitia fedha za uviko alisema kuwa kila darasa liligharimu kiasi cha shilingi milioni 20, ikilinganishwa na madarasa yaliyojengwa na Shanta Gold ambayo yamegharimu Tsh.milioni 28 kwa kila darasa.

“Kama mradi huu mngeshirikisha Halmashauri kwa kiasi kikubwa mngetumia Force Account na mgepata wakandarasi wa bei ndogo na fedha zingebaki zikafanya maendeleo mengine katika jamii. Niwashauri mshirikiane ipasavyo na Halmashauri kupanga aina ya miradi mnayotaka kuipeleka kwa jamii”. alisema Dkt. Mahenge.

Mkuu huyo wa mkoa mwenye uzoefu mkubwa serikalini akaipongeza Kampuni  ya shanta gold mining  kutumia zaidi ya Milioni 190 kupelekea jamii huduma ikiwemo ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na uchimbaji wa visima vya maji huduma ambazo zinafaidisha vijiji vya Mang’onyi, Sambaru, Mlumbi, Tupendane na Mwau.

Aidha, Dkt. Mahenge akaitaka jamii inayozunguka mgodi huo kutumia fursa na kuwa wabunifu kwa kuanzisha miradi mbalimbali ikiwemo ufugaji wa kuku na mama lishe pamoja na kuomba ajira katika kampuni hiyo kwa kuwa kadri mradi unavyokuwa ndivyo mahitaji yatakavyoongezeka.

 

Meneja wa Mradi huo kutoka kampuni ya uchimbaji wa madini ya Shanta gold  Kundael Mtiro wakati akiwasilisha taarifa ya mradi amesema mpaka kufikia sasa mradi ulitakiwa kufikia asilimia 46.14 katika utekelezaji wake lakini kwa sababu ambazo zimekuwa nje ya uwezo mpaka sasa utekelezaji wa mradi umefikia asilimia 43.62 .

Ameongeza kuwa kufikia  June, 2022 mradi utakuwa unakamilisha  robo ya nne ya mwaka ambapo wanategemea kwamba utakuwa umekamilika kwani mabomba yameshasimika katika maeno yote yanayohusika pamoja na uchimbaji wa visima, ujenzi wa ofisi na makazi umekamilika kwa asiliami 80.

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Jerry Muro akiwa miongozni mwa viongozi walioongozana na mkuu wa mkoa kwenye ziara hiyo akataja jinsi mgodi huo utakavyowanufaisha watu wanauzunguka mgodi huo hususani wakazi wa ikungi , Singida na taifa kwa ujumla ambapo utasisimua sekta nyingine za elimu barabara, zahanati na wananchi kupata ajira.

 

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com