Meneja Maswala Endelevu wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),Irene Mutiganzi akizungumza na wahudumu na wateja wa Meeda bar
Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),John Mtui akizungumza na wahudumu na wateja wa Meeda bar
Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),Patrick Swai akizungumza na wahudumu na wateja wa Soccer Bar
Maofisa wa TBL wakiwapiga darasa la unywaji kistaarabu wenye mabaa na wahudumu katika maeneo ya sinza jijini Dar es Salaam
……………………..
Kampuni ya Bia ya
TBL mwishoni mwa wiki iliendesha kampeni ya unywaji kistaarabu kwa
wamiliki wa mabaa na wafanyakazi wao lengo kuu likiwa ni kuwapatia elimu
hiyo ili waweze kuifikisha kwa watumiaji wa vinywaji vyenye kilevi.
Mbali
na kutoa elimu hii ambayo imelenga kufikishwa mikoa yote nchini pia
kampuni imeanza kuweka mabango ya kuhamasisha unywaji wa kistaarabu
katika maeneo yote vinapouzwa vinywaji.
Akiongea juu ya kampeni hiyo Meneja Mauzo wa TBL,John Mtui,alisema kuwa
unywaji wa kistaarabu ni moja ya ajenda ambayo kampuni imejipanga
kuhakikisha inafanikiwa na kuhakikisha watumiaji wa vilevi wanavitumia
kwa ajili ya kujenga afya zao na kupata burudani na sio kuleta athari
kwenye jamii na itafanyika nchini kote sambamba na kuwapatia wafanyabishara wanaoshirikiana na kampuni elimu ya ujasiriamali.
Mtui
aliongeza kusema kuwa TBL Group kwa muda mrefu imekuwa ikiendesha
kampeni za unywaji wa kistaarabu ambazo zimekuwa zikienda sambamba na
kuunga mkono jitihada za serikali za kutokomeza changamoto ya ajali nchini.
”Tumekuwa
na kampeni kubwa ya kuhamasisha madereva kutoendesha vyombo vya moto
wakiwa wamelewa,semina mbalimbali kuhusu madhara ya ulevi kwa makundi
mbalimbali,kutoa elimu ya unywaji wa kistaarabu kwa wadau wetu katika
biashara,kuweka nembo kwenye bidhaa zetu kuhusiana na kutowauzia
vinywaji vyenye kilevi watoto wenye umri mdogo usioruhusiwa kutumia
vinywaji”.Alisema.
Hatua
nyingine za kuhamasisha unywaji wa kistaarabu ambazo kampuni
imefanikisha alizitaja kuwa ni kuwapatia wafanyakazi mafunzo ya ndani
kuhusu madhara ya utumiaji mbaya wa vinywaji vyenye kilevi ambapo
hawaruhusiwi kuingia katika maeneo ya kazi wakiwa wametumia vinywaji
vyenye kilevi,kuzingatia kanuni za utangazaji wa bidhaa za kampuni zenye
kilevi,kushiriki semina na makongamano ya kampeni na kuongelea unywaji
wa kistaarabu.
Alisema suala
la kuhamasisha unywaji kistaarabu liko katika sera ya kampuni ya
‘’Dunia Maridhawa” ambayo inahamasisha kujenga jamii bora sambamba na
utunzaji wa mazingira. “Wiki iliyopita tuliadhimisha siku ya unywaji
kistaarabu ambayo ilizinduliwa na ABInBev mnamo mwaka 2010 na
tunawakaribisha wadau wote kushirikiana nasi katika kampeni za kuhamasisha unywaji wa kistaarabu na kutuunga mkono kwa kuzingatia matumizi mazuri ya vinywaji vyetu ili kufanikisha lengo lililokusudiwa’’.Alisisitiza.
0 comments:
Post a Comment