Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa
na Utamaduni, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akiangalia ngoma
ya kiutamaduni iliyokuwa ikipigwa na Kikundi cha Sanaa na Utamaduni
Tanzania (TaSUBA) katika banda lao wakati wa Tamasha la Utamaduni na
Sanaa Afrika Mashariki (JAMAFEST) linalofanyika mjini Kampala, Uganda 13
Septemba, 2017.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa
na Utamaduni, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akimsikiliza
mjasiriamali wa Tanzania kuhusu baadhi ya bidhaa zilizopo katika banda
lao wakati wa Tamasha la Utamaduni na Sanaa Afrika Mashariki (JAMAFEST)
linalofanyika mjini Kampala, Uganda 13 Septemba, 2017.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa
na Utamaduni, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) akipokea zawadi ya
shati toka kwa mjasiriamali wa Tanzania mara alipotembelea banda lao
wakati wa Tamasha la Utamaduni na Sanaa Afrika Mashariki (JAMAFEST)
linalofanyika mjini Kampala, Uganda 13 Septemba, 2017.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa
na Utamaduni, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (mwenye tai nyekundu)
akiangalia moja ya ubunifu wa picha iliyochongwa na mjasiriamali wa
Tanzania wakati wa Tamasha la Utamaduni na Sanaa Afrika Mashariki
(JAMAFEST) linalofanyika mjini Kampala, Uganda 13 Septemba, 2017. (PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-WHUSM)
……………………….
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa
na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe amewapongeza Wajasiriamali wa
Tanzania kwa ushiriki wao katika Tamasha la Utamaduni na Sanaa Afrika
Mashariki maarufu kama JAMAFEST.
Dkt. Mwakyembe ametoa pongezi hizo
leo mjini Kampala nchini Uganda katika viwanja vya Mashujaa Kololo
alipotembelea kujionea namna tamasha hilo lilivyopokelewa na wadau wake
walioiwakilisha Tanzania wakiwemo wajasiriamali toka vikundi mbalimbali,
vikundi vya ngoma, vikundi vya sanaa ya maigizo pamoja na baadhi ya
wasanii.
Katika tamasha hilo, Dkt.
Mwakyembe pia alipata fursa ya kutembelea baadhi ya mabanda ya
wajasiriamali hao pamoja na kuongea nao huku akijionea bidhaa mbalimbali
zinazouzwa na nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki jambo
ambalo limemfurahisha sana hususani kwa upande wa watu kutoka Tanzania
kwakuwa wamejaza mabanda yao kwa bidhaa kadha wa kadha.
“Tamasha hili linaonyesha utajiri
mkubwa wa sanaa, utamaduni pamoja na bidhaa tulizonazo kama nchi
wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, na hapa tumekutana kwasababu
tunabadilishana mawazo na kuonyeshana bidhaa mbalimbali za nchi zetu”,
alisema Dkt. Mwakyembe.
Aidha, katika ziara hiyo, Dkt.
Mwakyembe amewatoa wasiwasi wajasiriamali hao kuhusu suala la
upatikanaji wa masoko huku akiwaahidi kuwatafutia fursa ya kuwapeleka
wajasiriamali hao pamoja na bidhaa zao Bungeni mjini Dodoma ili ziweze
kupata soko kwa urahisi kupitia wabunge.
“Niwatoe wasiwasi wajasiriamali
wote wa Tanzania mliohudhuria hapa, nitahakikisha kuwa pindi tunaporudi
nyumbani nitatafuta wasaa wa kulishawishi Bunge la Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania ili nyie mpate nafasi ya kuleta bidhaa zenu katika viwanja
vya Bunge ili basi Wabunge wapate kujua haswa vitu vizuri mlivyonavyo
nah ii itawasaidia kuviuza kwa urahisi zaidi na kujipatia vipato vyenu”,
aliongeza Dkt. Mwakyembe.
Sambamba na hilo, Dkt, Mwakyembe
amewahakikishia wajasiriamali hao kuhusu suala la kujitangaza kupitia
vyombo vya habari akisema kwamba, atajitahidi kutoa ushawishi kwa vyombo
vya habari nchini ili viweze kuwapatia muda wa kuwatangaza
wajasiriamali hao ili wapate kujulikana ikiwemo shughuli wazifanyazo.
“Nitahakikisha kuwa siku mnapopewa
nafasi ya kuja viwanja vya Bunge basi mnapata muda wa kutosha katika
vyombo vya habari ili mpate kujulikana, hivyo kila mmoja wenu naamini
atapewa nafasi ya kufanya mahojiano kwa kujieleza shughuli azifanyazo na
mahali anapopatikana na hii itawasaidia kupata masoko zaidi toka kwa
watu mbalimbali”, alisema Dkt. Mwakyembe.
Kwa upande wao wajasiriamali hao
wameshukuru Waziri Mwakyembe kwa juhudi alizowafanyia hususani za
kuhakikisha kwamba wanahudhuria kwa kiwango kikubwa katika tamasha hilo,
lakini pia ahadi aliyowapa ya kuwapeleka Bungeni ili wakatangaze bidhaa
zao na kuwatangaza katika vyombo vya habari nchini.
Tamasha la JAMAFEST lilianzishwa
mwaka 2013 nchini Rwanda na baadhi ya Viongozi wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki ambapo kwa mwaka huu tamasha hilo linafanyika mjini Kampala
nchini Uganda ambapo pia tamasha hili linatarajiwa kufanyika tena katika
moja ya nchi mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) mwaka
2019.
0 comments:
Post a Comment