Makamu wa Rais
wa Hospitali ya Watoto ya Hunan nchini China akizungumza na washiriki wa
mafunzo ya siku 10 ya Madaktari na wauguzi wanaoshughulikia watoto
katika Hospitali ya Kivunge, Makunduchi na Mnazimmoja mafunzo
yanayofanyika Mnazimmoja Mjini Zanzibar.
Balozi mdogo wa
china aliepo Zanzibar XieXiawu akitoa hutuba katika ufunguzi wa mafunzo
ya siku 10 ya kuwajengea uwezo madaktari na wauguzi wanaofanyakazi wodi
za watoto za Hospitali ya Kivunge, Makunduchi na Kivunge.
Naibu Waziri
wa Afya Arusi Said Suleiman akifungua mafunzo ya madaktari na wauguzi
wanaoshughulikia watoto na kuimarisha utawala wa Hospitali, mafunzo
yanayofanyika Hospitali kuu ya Mnazimmoja.
Washiriki wa mafunzo kutoka
Hospitali ya Mnazimmoja, Kivunge na Makunduchi wakiwa pamoja na
wakufunzi wao kutoka Hospitali ya Hunan China wakifuatilia hotuba ya
ufunguzi iliyotolewa na Naibu Waziri wa Afya Bi. Arusi Said Suleiman
(hayupo pichani).
Picha na Makame Mshenga.
…………………………
Na Ramadhani Ali – Maelezo
Makamu wa Raiswa Hospitali ya
watoto ya Hunan Chini China Zhu Lihui ameahidi kuwa Hospitali hiyo
itaendelea kushirikiana na Hospitali ya Mnazimmoja ya Zanzibar
kuwajengea uwezo wafanyakazi na kuimarisha Utawala wa Hospitali.
Zhu ameeleza hayo wakati wa
ufunguzi wa mafunzo ya siku kumi yanayowashirikisha madaktari na wauguzi
25 wanaoshughulikia watoto kutoka Hospitali ya Mnazimmoja, Kivunge na
Makunduchi.
Amesema Hospitali ya watoto ya
Hunan imewahi kutoa mafunzo kwa wafanyakazi 26 katika vipindi tofauti
nchini China imeamua kufanya mafunzo Zanzibar kwa kushirikiana na Wizara
ya Afya iliwafanya kazi wengi waweze kufaidika.
Ameeleza matarajio yake kuwa
wafanyakazi waliopata nafasi ya kushiriki mafunzo hayo wataenda
kuwaelimisha wafanyakazi wenzao ambao hawakubahatika kushiriki.
Aidha amesema kuja kwamadaktari
bingwa kutoka jimbo la Hunan kutoa mafunzo hapa Zanzibar kutaongeza
mashirikiano kati ya Hospitali ya Mnazimmoja na kubadilishana uzoefu
katika kuimarisha afya za wananchi na kuimarisha masuala ya utawala.
Balozi mdogo wa China aliepo
Zanzibar Xie Xiawu amesema ushirikiano baina ya China na Zanzibar
niwamuda mrefu na nchi yake itaendelea kusaidia Zanzibar katika
kuimarisha na kukuza maendeleo ya wananchi.
Alisema mafunzo yatakayotolewa na
wataalamu kutoka Hospitaliya watoto ya Hunan yatawajengea uwezo
watendaji wa wodi za watoto na kuimarisha afya ya mama baada ya
kujifungua na watoto wanaozaliwa.
Akifungua mafunzo hayo
yanayofanyika Hospitali mpya ya wazazi ya Mnazimmoja, Naibu Waziri wa
Afya Harusi Saidi Suleiman aliishukuru Hospitali ya watoto ya Hunan kwa
kusaidia kuwaongezea ujuzi wafanyakazi wanaoshughulikia matatizo ya
watoto na kuimarisha utawalawa Hospitali.
Aliwataka washiriki wa mafunzo
hayo kuwa wasikivu na kufuatilia kwa karibu masomo watakayo someshwa ili
nao kuja kuwa walimu kwa wengine baada ya kumaliza na kuwawezesha
wataalamu wa China kusomesha kada nyengine za afya.
0 comments:
Post a Comment