MKUU wa wilaya ya Rufiji ,Juma
Njwayo wa kwanza kulia aliyenyoosha kidole ,akitoa maelekezo kwa mganga
mfawidhi wa zahanati ya Utunge ,Emmanuel Edmond wa nne kutoka kulia
,wakati wa ziara yake ya kutembelea zahanati na vituo vya afya
kufuatilia fedha za mpango wa malipo ya matokeo ya ufanisi wa kazi
kwenye maeneo yao (RBF)ili kuboresha huduma .
MKUU wa wilaya ya Rufiji ,Juma Njwayo wa kwanza kulia akizungumza jambo na kaimu mganga mkuu wa wilaya ya Rufiji, Didas Asenga. Picha na Mwamvua Mwinyi
………………………
Na Mwamvua Mwinyi,Rufiji
MKUU
wa wilaya ya Rufiji ,Juma Njwayo amewaagiza waganga wafawidhi wa
zahanati na vituo vya afya wilayani hapo ,kufuata miongozo na kusimamia
fedha za mpango wa malipo ya matokeo ya ufanisi wa kazi kwenye maeneo
yao (RBF)ili kuboresha huduma za afya.
Aidha
amewaasa watumishi hao kuachana na tabia ya kuingiza siasa kwenye
majukumu yao hali inayosababisha kukwama kwa jitihada za kuleta
mabadiliko katika sekta hiyo.
Njwayo
,amekemea baadhi ya wauguzi hasa wodi ya uzazi ambao wamekuwa
wakiwatolea lugha zisizoridhisha na maneno machafu akinamama wanaokwenda
kujifungua.
Mkuu
huyo wa wilaya ,amemtaka na kaimu mganga mkuu wa wilaya ya Rufiji Didas
Asenga,kusimamia maagizo na maelekezo hayo aliyoyatoa pamoja na
kuhakikisha afisa afya anaongeza kasi ya kuweka mazingira safi kwani
maeneo mengi hususan baadhi ya zahanati,usafi hauridhishi.
Aliyasema
hayo wakati wa ziara yake aliyoianza kutembelea vituo vya afya na
zahanati 28 zilizopo wilayani Rufiji ,kufuatilia fedha za awali
zilizotolewa katika mpango wa RBF kiasi cha sh .mil.10 kila zahanati .
Njwayo
alisema, wizara imeleta mpango huo kwa dhamira njema lakini amegundua
kuna changamoto kubwa kwa baadhi ya zahanati kushindwa kufuata maelekezo
na miongozo waliyopatiwa.
“Lipo
tatizo la kutofuata maelekezo ya mradi suala litakalosababisha kukosa
fedha nyingi kwa ajili ya mradi endapo asilimia zao hazijafikia,
wanajipotezea point.”alisema
Hata
hivyo alisema,hatua inayofuata baada ya kutolewa mil.10 ni kuongezwa
fedha kila zahanati kulingana na kiwango cha malipo ya ufanisi
zilizoonekana .
“Nimeanza
ziara yangu leo,na nimepitia zahanati ya Tapika ambayo katika ukaguzi
uliofanywa na maofisa wa mradi wametoa asilimia 49,Ngarambe asilimia
29,Kingupira 24,Utunge 20 na zahanati ya Chumbi imejitahidi imepata
asilimia 75”alifafanua Njwayo.
Njwayo alieleza ,atakaezembea atachukuliwa hatua kwani mradi ulipoanza walipewa miongozo na maelekezo kama hawayafuatilii ina maana wanakiuka kwa makusudi.
Aliwataka wafanyakazi wa zahanati na vituo vya afya kujenga umoja na ushirikiano na kamati za afya ili kamati ziache kujisahau kushirikisha na jamii kwa kuitisha mikutano kuwaeleza masuala ya afya na umuhimu wa bima za afya .
Akizungumzia maadili kwa watumishi
wa afya,Njwayo alisema,lazima kuheshimu wagonjwa na kutoa kauli za staha
na kuwa wasiri pasipo kutoa aibu za wagonjwa mitaani.
Alisema sio utaratibu wa namna ya
kutibia wagonjwa na kama kuna mtumishi atabainika kukiuka hayo
atamchukulia hatua za kimaadili.
Kwa upande wake kaimu mganga mkuu wilaya ya Rufiji,Didas Asenga ,alisema amepokea maagizo na maelekezo yote aliyopatiwa.
Anasema
mpango wa malipo kwa ufanisi umeleta matokeo chanya kwani awali
zahanati nyingi zilikuwa na miundombinu chakavu,nyingine zilikuwa hazina
vyoo,uhaba wa madawa,kukosekana vichomea taka lakini kwa sasa baada ya
kupatiwa mil.10 kwa kila zahanati imeweza kuboresha huduma hizo.
Asenga alielezea,zipo changamoto zinazojitokeza ikiwemo baadhi ya zahanati kukosa uelewa wa hatua za manunuzi na mahesabu .
Alisema
,kunahitajika wahasibu wasaidizi katika kila zahanati ili kusimamia
fedha zijazo na kuweka kumbukumbu kitaalamu na hatimae kuondokana na
mapungufu yaliyopo.
Asenga alibainisha,mafunzo na elimu ya kutosha inahitajika kwa wakuu wa vituo vya afya ili kupunguza matatizo hayo.
Nae
mwenyekiti wa kijiji cha Nyamwage ,Ibrahim Said alisema mpango huo ni
mzuri kwakuwa umeweza kuimarisha huduma ya afya kwa jamii.
0 comments:
Post a Comment