UZALENDO KWANZA wakiongozwa na mkuu wa Wilaya ya Handeni, Mhe. Godwin
Gondwe wakielekea katika kijiji cha Kitumbi wilaya ya Handeni mkoa wa
Tanga, ambapo walipatiwa Mashamba yenye ukubwa wa hekari 282 za ardhi
kwa ajili ya uwekezaji wa Kilimo. Picha zote na Kajunason/MMG-Handeni.
Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Mhe. Godwin Godwe akiongea mara baada ya
kuwakabidhi ardhi yenye ukubwa wa hekari 282 katika kijiji cha kitumbi
kwa wasanii na wadau wengine wanaofanya kampeni ya UZALENDO KWANZA.
Tukio hilo lilifanyika kijijini Kitumbi, Muheza – Tanga mwishoni mwa
wiki iliyopita.
Mwenyekiti wa UZALENDO KWANZA, Msanii Steve Nyerere akitoa shukrani
zake za pekee kwa mkuu wa Wilaya ya Handeni, Mhe. Godwin Gondwe mara
baada ya kuwakaribisha wana- UZALENDO KWANZA na kuwapatia hekari 282 za
ardhi kwa ajili ya uwekezaji wa kilimo katika kijiji cha Kitumbi wilaya
ya Handeni mkoa wa Tanga.
Diwani wa Kata ya Kitumbi, Charles Abeid akiwakaribisha wasanii na wadau wengine wanaofanya kampeni ya UZALENDO KWANZA.
Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Mhe. Godwin Gondwe akiwatambulisha viongozi wa kijiji cha Kitumbi, Handeni -Tanga.
0 comments:
Post a Comment