METDO Tanzania

METDO Tanzania

Friday, August 18, 2017

Waziri Ummy Mwalimu awataka watoa huduma kituo cha afya Matai wilayani Kalambo kutoa huduma bora kwa wanawake wajawazito

IMG_2257
Msafara huo wakiangalia jengo la maabara(halipo pichani) wakati wa ukaguzi wa majengo yaliyopo kituo cha afya Matai  Kushoto ni waziri Ummy Mwalimu,katikati ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Dkt.Boniface Kasulu na kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Julieth Binyura(Picha zote na Wizara ya Afya)
IMG_2240
Waziri Ummy Mwalimu akiongea na baadhi ya akina mama waliofika kupata huduma kwenye kituo hicho cha afya 
IMG_2243
Mkuu wa Wilaya ya ya Kalambo Julieth Binyuru akisalimiana na akina mama hao waliokuwa wakisubiri kuwajulia hali wagonjwa wao waliolazwa kwenye kituo vha afya cha Matai
IMG_2245
Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto akimjulia hali mama aliyejifungua kwenye wodi ya wazazi kituoni hapo
IMG_2250
-Baadhi ya Watumishi wa Kituo cha afya cha Matai wakimsikiliza Waziri huyo wakati aluipofanya ziara kwenye kituo cha afya kwa ajili ya kujione hali ya utoaji huduma za afya Mkoani Rukwa
IMG_2191
Afisa Muuguzi Msaidizi Darous Bakari akisoma taarifa ya kituo cha afya cha Matai Wilayni Kalambo wakati wa mkutano wa Waziri wa Afya alipokuwa akizungumza na watumishi wa kituo hicho.

Na.WAMJW-Kalambo 

Waziri wa Afya,Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amewataka watoa  huduma za afya katika kituo cha afya cha Matai wilayani Kalambo kutoa huduma bora kwa wanawake wajawazito.

Rai hiyo imetolewa jana na Waziri huyo alipokuwa kwenye ziara ya kikazi wilayani hapo na kutembelea hospitali hiyo pamoja na kuongea na watumishi wa sekta ya afya kujua changamoto zinazowakabili.

Alisema wajawazito wanapaswa kupata huduma bora kila wanapofika kliniki kila mwezi kwa kuangaliwa mfano dalili za kifafa cha mimba ,wigi wa proteini pamoja na viatarishi vingine  vinavyoweza kusababisha  uzazi pingamizi na hivyo kupelekea vifo kwa mama au mtoto wakatiwa kujifungua

“Nawapongeza sana kwa kutenga dirisha la wazee ila kusiwepo tu dirisha bali muwape dawa wazee wasio kuwa na uwezo,hivyo kama kuwakatia mfuko wa bima ya jamii (CHF)ni gharama basi wapatieni vitambulisho vya matibabu bure ili wazee wakija kwenye matibabu wasije na barua za watendaji wa vijiji”

Kwa upande wa madawa Waziri Ummy amewaambia watendaji hao hakuna masharti magumu ya ununuzi wa madawa na vifaa tiba kwa kutumia pesa za CHF“nimeshawaambia MSD ndani ya masaa ishirini na nne umeagiza vitu MSD hana,ndani ya masaa hayo kama hana unaruhusiwa kwenda kununua unapotaka kwenda”hivyo ni vyema wakapitisha wadhaburi watakaokuwa wananunua.

“Tangu serikali hii iingie madarakani imefanya mabadiliko makubwa katika upatikanaji wa dawa kwa kuongezwa bajeti ya dawa kwa asilimia kubwa,hizi changamoto ndogondogo zipo ila mwisho wa siku wananchi wanahitaji dawa,hivyo kuhakikisha dawa zile muhimu zinapatikana wakati wote.

Hata hivyo amewataka kuwapa kipaumbele wale wanaotumia bima ya afya,nataka kuona mnaongeza wananchi watakaotumia bima ya afya kwenye matibabu ili kuweza kutatua changamoto za sekta ya afya

Upande wa Malaria Waziri Ummy vipimo vya haraka vya malaria vya MRTD ni bure pamoja na dawa ya kutibu Malaria’ALU’ ni bure”asije kuwaambia mtu kipimo hicho utoe pesa,sindano kama mtu amezidiwa na maralia kali ni bure”alisisitiza Waziri Ummy

Akiongelea ugonjwa wa Kifua Kikuu”TB” Waziri huyo alisema ni wakati wa kuwaambiwa watu Tb inatibika kwani katika kila watu mia moja wanaoumwa kifua kikuu na kutumia dawa watu tisini wanapona kabisa na wanaendelea na shughuli zao.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com