Msafara huo wakiangalia jengo la
maabara(halipo pichani) wakati wa ukaguzi wa majengo yaliyopo kituo cha
afya Matai Kushoto ni waziri Ummy Mwalimu,katikati ni Mganga Mkuu wa
Mkoa wa Rukwa Dkt.Boniface Kasulu na kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kalambo
Julieth Binyura(Picha zote na Wizara ya Afya)
Waziri Ummy Mwalimu akiongea na baadhi ya akina mama waliofika kupata huduma kwenye kituo hicho cha afya
Mkuu
wa Wilaya ya ya Kalambo Julieth Binyuru akisalimiana na akina mama hao
waliokuwa wakisubiri kuwajulia hali wagonjwa wao waliolazwa kwenye kituo
vha afya cha Matai
Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto akimjulia hali mama aliyejifungua kwenye wodi ya wazazi kituoni hapo
-Baadhi
ya Watumishi wa Kituo cha afya cha Matai wakimsikiliza Waziri huyo
wakati aluipofanya ziara kwenye kituo cha afya kwa ajili ya kujione hali
ya utoaji huduma za afya Mkoani Rukwa
Afisa
Muuguzi Msaidizi Darous Bakari akisoma taarifa ya kituo cha afya cha
Matai Wilayni Kalambo wakati wa mkutano wa Waziri wa Afya alipokuwa
akizungumza na watumishi wa kituo hicho.
Na.WAMJW-Kalambo
Waziri wa Afya,Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy
Mwalimu amewataka watoa huduma za afya katika kituo cha afya cha Matai
wilayani Kalambo kutoa huduma bora kwa wanawake wajawazito.
Rai hiyo imetolewa jana na Waziri huyo alipokuwa kwenye ziara
ya kikazi wilayani hapo na kutembelea hospitali hiyo pamoja na kuongea
na watumishi wa sekta ya afya kujua changamoto zinazowakabili.
Alisema wajawazito wanapaswa kupata huduma bora kila
wanapofika kliniki kila mwezi kwa kuangaliwa mfano dalili za kifafa cha
mimba ,wigi wa proteini pamoja na viatarishi vingine vinavyoweza
kusababisha uzazi pingamizi na hivyo kupelekea vifo kwa mama au mtoto
wakatiwa kujifungua
“Nawapongeza sana kwa kutenga dirisha la wazee ila kusiwepo
tu dirisha bali muwape dawa wazee wasio kuwa na uwezo,hivyo kama
kuwakatia mfuko wa bima ya jamii (CHF)ni gharama basi wapatieni
vitambulisho vya matibabu bure ili wazee wakija kwenye matibabu wasije
na barua za watendaji wa vijiji”
Kwa upande wa madawa Waziri Ummy amewaambia watendaji hao
hakuna masharti magumu ya ununuzi wa madawa na vifaa tiba kwa kutumia
pesa za CHF“nimeshawaambia MSD ndani ya masaa ishirini na nne umeagiza
vitu MSD hana,ndani ya masaa hayo kama hana unaruhusiwa kwenda kununua
unapotaka kwenda”hivyo ni vyema wakapitisha wadhaburi watakaokuwa
wananunua.
“Tangu serikali hii iingie madarakani imefanya mabadiliko
makubwa katika upatikanaji wa dawa kwa kuongezwa bajeti ya dawa kwa
asilimia kubwa,hizi changamoto ndogondogo zipo ila mwisho wa siku
wananchi wanahitaji dawa,hivyo kuhakikisha dawa zile muhimu zinapatikana
wakati wote.
Hata hivyo amewataka kuwapa kipaumbele wale wanaotumia bima
ya afya,nataka kuona mnaongeza wananchi watakaotumia bima ya afya kwenye
matibabu ili kuweza kutatua changamoto za sekta ya afya
Upande wa Malaria Waziri Ummy vipimo vya haraka vya malaria
vya MRTD ni bure pamoja na dawa ya kutibu Malaria’ALU’ ni bure”asije
kuwaambia mtu kipimo hicho utoe pesa,sindano kama mtu amezidiwa na
maralia kali ni bure”alisisitiza Waziri Ummy
Akiongelea ugonjwa wa Kifua Kikuu”TB” Waziri huyo alisema ni
wakati wa kuwaambiwa watu Tb inatibika kwani katika kila watu mia moja
wanaoumwa kifua kikuu na kutumia dawa watu tisini wanapona kabisa na
wanaendelea na shughuli zao.
No comments:
Post a Comment