Naibu Waziri wa Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe.Angelina Mabula amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri Mkoani
Simiyu kuwasimamia watumishi wa Idara ya
Ardhi na kuhakikisha wanapima maeneo na
kutoa hati miliki kwa wananchi.
Mhe.Mabula
ameyasema hayo wakati wa ziara yake Mkoani Simiyu ambayo imelenga kufuatilia utekelezaji
wa maelekezo mbalimbali aliyoyatoa wakati wa ziara yake Novemba 2017, mwenendo
wa ukusanyaji wa kodi za ardhi na kukagua
Jengo la Kanda ya Ardhi Simiyu itakayohudumia Mikoa ya Simiyu,Shinyanga na
Mara,
“Mtumishi
aliyeajiriwa kama surveyor (mpima ardhi) hana sababu za kukaa ofisini kuanzia
saa 1:30 asubuhi mpaka saa 9:30 alasiri wakati kazi zake nyingi ziko uwandani;
Mwisho atajikuta amepima viwanja 58 mwaka mzima, maana yake ni kwamba atakuwa hajajua
wajibu wake, wakurugenzi badilikeni katika kuwasimamia watumishi wa sekta ya
ardhi” amesema Mabula
Amesema ikiwa
Watumishi wa Idara ya Ardhi wakitimiza wajibu wao Ardhi ikapimwa, wananchi wakapewa
hati miliki ya maeneo yao ya viwanja na mashamba; migogoro itapungua, Serikali itakusanya
maduhuli kupitia kodi ya Ardhi na uendelezaji wa miji utafanyika katika mpango
mzuri
Pamoja na kupima
maeneo na kutoa hati miliki, Mhe.Naibu Waziri amesema Idara ya Ardhi inapaswa
kuhakikisha wananchi waliomilikishwa maeneo wanajenga kwa kuzingatia sheria
Namba 8 ya mwaka 2007 ya Mipango Miji, ili kuepukana na ujenzi holela
unaopelekea kuwa na miji isiyopangwa.
Aidha, Mhe.Naibu
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, amesisitiza maeneo yote ya
Taasisi za Serikali yapimwe na kutolewa hati miliki ili kuyalinda na uvamizi.
Sanjali na hilo,
Mhe.Naibu Waziri amewataka wataalam wa Ardhi kukusanya maduhuli ya Serikali yatokanayo
na kodi za ardhi kwa kutumia mifumo ya Kielektroniki iliyowekwa katika
kufuatilia na kuhakikisha wananchi wote wanaostahli kulipa kodi ya ardhi
wanalipa kwa wakati.
Naibu Waziri
ameelekeza Kamati za Halmashauri zinazosimamia Ardhi zihakikishe zinaifanya
agenda ya Makusanyo ya maduhuli kuwa ya kudumu katika vikao vyao vya kila robo,
ili kila wanapokutana itolewe taarifa ya hali ya makusanyo, wananchi waliopewa
notisi na wale wanaotakiwa kupelekwa katika mabaraza ya Ardhi ya Wilaya kwa
kushindwa kulipa kodi ya ardhi kwa wakati.
Akiwasilisha
taarifa ya Wilaya ya Bariadi Mkuu wa Wilaya hiyo, Mhe.Festo Kiswaga amesema Halmashauri
zote mbili zinazounda Wilaya ya Bariadi zinaendelea na kuhamasisha wananchi
kupima maeneo yao na kupata hati miliki ili kuongeza ukusanyaji wa maduhuli ya
Serikali kupitia kodi ya Ardhi, ambapo Halmashauri ya Wilaya Bariadi pekee kwa
mwaka 2017/2018 inatarajia kupima viwanja 2400 katika Vituo vya Kibiashara vya
Nkololo,Dutwa na Ngulyati.
Naye Kaimu
Kamishna wa Ardhi Msaidizi wa Kanda, Makwasa Biswalo amesema Mtalaam kutoka
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi amefika Mkoani Simiyu kwa ajili
ya kutoa mafunzo ya mfumo wa ukusanyaji wa kodi za Ardhi, kwa watumishi wa Halmashauri zote ambao
utawawezesha kutengeneza ankara (bill) ya makusanyo ya kodi na tozo zote.
Kwa upande wake
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka ameshukuru Wizara ya Ardhi kwa kuona
Umuhimu wa kuanzisha Kanda ya Ardhi ya Simiyu na akaomba Wizara ifanye
utaratibu wa kumleta Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi la Maswa kutokana na
aliyekuwepo kasimamishwa kazi, hali iliyopelekea mashauri mengi kutofanyiwa
kazi.
Msajili Msaidizi
wa Baraza la Ardhi Kanda ya Ziwa, Dorothy Moses amesema kuanzia mwezi Septemba
2017 atakuwepo Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi na Nyumba la Maswa ambaye atasikiliza kesi, ambapo pia ameleeza
kuwa Wizara ina mpango wa kuanzisha mabaraza mawili ya Ardhi na Nyumba katika
Wilaya ya Bariadi na Busega ambayo yataanzishwa muda wowote baada ya kupatikana
majengo kwa ajili ya Ofisi.
Naibu
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe.Angelina Mabula(Mb) yuko
katika ziara ya siku mbili Mkoani Simiyu ambapo akiwa Mjini Bariadi amefanya
kikao na Viongozi, wataalam wa Ardhi na
Watendaji wa Kata,Mitaa na Vijiji wa Halmashauri ya Mji Bariadi na Halmashauri
ya Wilaya Bariadi kilichofanyika Mjini Bariadi.
Naibu Waziri wa Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Mhe.Angelina Mabula(Mb) (wa pili
kushoto)akizungumza na viongozi, watumishi wa Idara ya Ardhi na Watendaji wa
Kata, Mitaa na Vijiji wa Wilaya ya Bariadi wakati wa ziara yake Mkoani Simiyu.
Mkurugenzi wa Wilaya ya
Bariadi(kushoto) akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo
ya Makazi , Mhe.Angelina Mabula(Mb)(kulia) kuhusu jengo lililoandaliwa kwa
ajili ya Ofisi ya Ardhi Kanda ya Simiyu ambayo inatarajia kuanza kazi hivi
karibuni, ambayo itahudumia mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga.
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akizungumza kabla ya kumkaribisha Naibu
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Mhe.Angelina
Mabula(Mb)azungumze na Viongozi wa Mkoa na Wilaya ya Bariadi(hawapo pichani)
kabla ya kuanza ziara yake Mkoani humo.
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akizungumza kabla ya kumkaribisha Naibu
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Mhe.Angelina
Mabula(Mb)azungumze na Viongozi wa Mkoa na Wilaya ya Bariadi(hawapo pichani)
kabla ya kuanza ziara yake Mkoani humo.
Mkuu wa Wilaya ya
Bariadi, Mhe.Festo Kiswaga akiwaasilisha taarifa ya Wilaya hiyo kwa Naibu
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Mhe.Angelina Mabula(Mb)(wa
tatu kushoto)wakati akiwa katika Ziara ya siku Mbili Mkoani Simiyu.
Mkurugenzi wa mji wa
Bariadi, Ndg.Melkizedek Humbe akichangia hoja katika kikao kati ya Naibu Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Mhe.Angelina Mabula(Mb), viongozi,
watumishi wa Idara ya Ardhi na Watendaji wa Kata, Mitaa na Vijiji wa Wilaya ya
Bariadi, kilichofayika mjini Bariadi
wakati wa ziara ya Naibu Waziri huyo
Mkoani Simiyu.
Mkurugenzi wa mji wa
Bariadi, Ndg.Melkizedek Humbe akichangia hoja katika kikao kati ya Naibu Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Mhe.Angelina Mabula(Mb), viongozi,
watumishi wa Idara ya Ardhi na Watendaji wa Kata, Mitaa na Vijiji wa Wilaya ya
Bariadi, kilichofayika mjini Bariadi
wakati wa ziara ya Naibu Waziri huyo
Mkoani Simiyu.
Mkurugenzi wa mji wa
Bariadi, Ndg.Melkizedek Humbe akitoa maelekezo kwa Naibu Waziri wa Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Mhe.Angelina Mabula(Mb) wakati alipotembelea Ofisi
ya Idara ya Ardhi ya Halamashauri hiyo kujionea namna inavyokusanya mapato
yatokanayo na Ardhi, wakati wa ziara yake Mkoani Simiyu.
Msajili Msaidizi wa
Baraza la Ardhi Kanda ya Ziwa, Dorothy Moses akitoa ufafanuzi juu ya hoja
mbalimbali zilizowasilishwa na watumishi wa Idara ya Ardhi katika kikao cha Naibu
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Mhe.Angelina Mabula(Mb) na
watumishi hao mjini Bariadi.
Kaimu Kamishna wa Ardhi
Msaidizi wa Kanda, Makwasa Biswalo akitoa ufafanuzi juu ya hoja mbalimbali
zilizowasilishwa na watumishi wa Idara ya Ardhi katika kikao cha Naibu Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Mhe.Angelina Mabula(Mb) na watumishi
hao mjini Bariadi.
Kaimu Kamishna wa Ardhi
Msaidizi wa Kanda, Makwasa Biswalo akitoa ufafanuzi juu ya hoja mbalimbali
zilizowasilishwa na watumishi wa Idara ya Ardhi katika kikao cha Naibu Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Mhe.Angelina Mabula(Mb) na watumishi
hao mjini Bariadi.
Mkuu wa Wilaya ya
Bariadi, Mhe.Festo Kiswaga akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi , Mhe.Angelina Mabula(Mb)
kuhusu eneo la uwanja wa ndege wa Kidulya lililokuwa limevamiwa na
mwananchi mmoja na namna Serikali ilivyolishughulikia, wakati alipolitembelea
eneo hilo akiwa katika ziara yake mkoani Simiyu.
Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Mji Bariadi, Melkizedek Humbe(kulia) akimweleza Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi , Mhe.Angelina Mabula(Mb) hatua
zilizochukuliwa na Halmashauri dhidi ya mwananchi aliyevamia eneo la uwanja wa
ndege Kidulya, wakati alipolitembelea eneo hilo akiwa katika ziara yake mkoani
Simiyu.
Mwanasheria wa
Halmashauri ya Mji, Ndg.Speratus Boniphace akichangia hoja katika kikao cha Naibu
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Mhe.Angelina Mabula(Mb) na watumishi
wa Idara ya Ardhi na Watendaji wa Kata, Mitaa na Vijiji wa Wilaya ya Bariadi,
kilichofanyika Mjini Bariadi wakati wa ziara ya Naibu Waziri huyo Mkoani Simiyu.
Baadhi ya watumishi wa
Idara ya Ardhi Mkoa na Wilaya na Watendaji wa Kata, Mitaa na Vijiji wa Wilaya
ya Bariadi wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ,
Mhe.Angelina Mabula(Mb) (hayupo pichani) katika kikao kilichofanyika Mjini
Bariadi wakati wa ziara yake Mkoani Simiyu.
Naibu Waziri wa Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Mhe.Angelina Mabula(Mb) akitoa maelekezo mara
baada ya kutembelea eneo la Uwanja wa Ndege wa Kidulya Mjini Bariadi wakati wa
ziara yake Mkoani Simiyu.
Mtaalam kutoka
Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi, Ndg. Martha Zongo hoja katika kikao cha Naibu
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Mhe.Angelina Mabula(Mb) na watumishi
wa Idara ya Ardhi na Watendaji wa Kata, Mitaa na Vijiji wa Wilaya ya Bariadi,
kilichofanyika Mjini Bariadi wakati wa ziara ya Naibu Waziri huyo Mkoani Simiyu.
Katibu Tawala Msaidizi
ehemu ya Utawala na Rasilimaliwatu wa Sekretarieti ya Mkoawa Simiyu(ambaye
alimwakilisha Katibu Tawala Mkoa) akiwatambulisha viongozi na watumishi
mbalimbali walioshiriki katika ziara ya Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi , Mhe.Angelina Mabula(Mb)
Naibu Waziri wa Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Mhe.Angelina Mabula(Mb)(wa tatu kushoto) akiwa
katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya
Bariadi na baadhi ya wataalam wa Ofisi ya Ardhi Kanda ya Ziwa wakati wa ziara
yake Mkoani Simiyu.
Naibu Waziri wa Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Mhe.Angelina Mabula(Mb)(wa tatu kushoto) akiwa
katika picha ya pamoja na baadhi ya Madiwani wa Halmashauri ya Mji Bariadi,
wakati wa ziara yake Mkoani Simiyu.
Naibu Waziri wa Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Mhe.Angelina Mabula(Mb)(wa tatu kushoto) akiwa
katika picha ya pamoja wakuu wa idara wa Halmashauri ya Mji na Wilaya ya
Bariadi, wakati wa ziara yake Mkoani Simiyu.
|
0 comments:
Post a Comment