METDO Tanzania

METDO Tanzania

Tuesday, September 5, 2017

ASKOFU SANGU AWATAKA VIJANA WASIKUBALI KUTUMIWA KULETA CHUKI, FITINA NA MAFARAKANO

Mhashamu Askofu  wa Kanisa  Katoliki Jimbo la SHINYANGA Liberatus Sangu amewataka Vijana kutokubali kutumiwa kuleta vurugu, chuki na mafarakano hapa nchini.

Askofu Sangu ametoa wito huo wakati wa Ibada ya Sakramenti ya Kipaimara iliyofanyika katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu John Mjini Bariadi.

“......Maandiko Matakatifu yanasema Vijana wana nguvu;  kwa hiyo nawasihi vijana popote pale mlipo muwe chimbuko la Upendo, furaha na amani; watu wengine wasitumie nguvu zenu vijana kuleta chuki, fitina na mafarakano, muwe macho” alisema Askofu Sangu.

Askofu Sangu amewaasa waumini wa Kanisa hilo kuishi maisha mema ambayo hayatakuwa chanzo cha mateso kwa watu wengine katika familia, jumuiya , jamii wanaoishi na Taifa kwa ujumla.

Aidha, amewataka Watanzania wote kupinga na kukemea mauaji ya watu wenye ualbino kwa kuwa wanayo haki ya kuishi kama watu wengine na watu wote wameumbwa kwa mfano wa Mungu.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka ametoa wito kwa Kanisa kuwa na mtazamo wa  kuisaidia nchi katika kupambana na tatizo la ajira hususani  kwa vijana.

Ameongeza kuwa ni vema Kanisa liyavae maneno ya Mhe.Rais kuhusu Ujenzi wa Tanzania ya Uchumi wa Kati na kuona namna linavyoweza kushiriki katika kufikia Tanzania Mpya, kwa kuimarisha  Idara za Kanisa na Vyama vya Kitume na kuzijenga idara na vyama hivyo katika  mtazamo wa Kiujasiriamali.

“Kanisa lione namna gani WAWATA tulionao wanakuwa WAWATA wa miradi, VIWAWA wanakuwa wa miradi, TYCS wa miradi, lakini sasa Vyama vyetu vya Kitume navyo pia vianze kujielekeza kusaidia Kanisa kwenye eneo la miradi”amesema Mtaka.

Mtaka amesema upo umuhimu wa kufanya semina za Ujasiriamali kwa vijana, wanawake na Vyama vya Kitume katika Kanisa  na waumini wote kwa ujumla ili kuwa na waumini waliojengwa kiuchumi na wanaoendana na mtazamo wa Serikali ya Awamu ya Tano ya kufikia Uchumi wa Kati.
Akiwa katika Ziara yake Mkoani Simiyu, Mhashamu Askofu  wa Kanisa  Katoliki Jimbo la SHINYANGA Liberatus Sangu , Jumamosi Septemba 02 alizindua Parokia mpya ya Mtakatifu Luka iliyopo  Mjini BARIADI,  sambamba na kutoa kipaimara na leo ametoa kipaimara kwa vijana 164, katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu John Mjini Bariadi.
Mhashamu Askofu  wa Kanisa  Katoliki Jimbo la SHINYANGA Liberatus Sangu akiongoza Ibada ya Sakramenti ya Kipaimara katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu John Mjini Bariadi.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akizungumza na Waumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu John Mjini Bariadi katika Ibada ya Sakramenti ya Kipaimara iliyoongozwa na Mhashamu Askofu  wa Kanisa  Katoliki Jimbo la SHINYANGA Liberatus Sangu.
Mhashamu Askofu  wa Kanisa  Katoliki Jimbo la SHINYANGA Liberatus Sangu akiwapaka mafuta vijana wa Kipaimara katika Ibada ya Sakramenti ya Kipaimara iliyofanyika  katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu John Mjini Bariadi.

Mhashamu Askofu  wa Kanisa  Katoliki Jimbo la SHINYANGA Liberatus Sangu akiwabariki vijana wa Kipaimara katika Ibada ya Sakramenti ya Kipaimara iliyofanyika  katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu John Mjini Bariadi.
Baadhi ya Vijana waliopata Sakramenti ya Kipaimara katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu John Mjini Bariadi wakiimba katika ibada .
Kwaya ya Shirikisho ikiimba  katika Ibada ya Sakramenti ya Kipaimara iliyofanyika  katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu John Mjini Bariadi.
Mhashamu Askofu  wa Kanisa  Katoliki Jimbo la SHINYANGA Liberatus Sangu  akiingia katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu John Mjini Bariadi ambapo aliongoza Ibada ya Sakramenti ya Kipaimara.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka (mwenye shati jeupe) na Mkewe Neema Mbiha(kulia) wakifuatilia mahubiri wakati wa Ibada ya Sakramenti ya Kipaimara katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu John Mjini Bariadi iliyoongozwa na Mhashamu Askofu  wa Kanisa  Katoliki Jimbo la SHINYANGA Liberatus Sangu.
Vijana wa Kipaimara (wenye sare ya rangi nyekundu) katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu John Mjini Bariadi wakiingia  Kanisani kwa ajili ya ibada ya Sakramenti hiyo, ambayo iliongozwa Mhashamu Askofu  wa Kanisa  Katoliki Jimbo la SHINYANGA Liberatus Sangu.
Mhashamu Askofu  wa Kanisa  Katoliki Jimbo la SHINYANGA Liberatus Sangu  akizindua Kitabu cha “MWANZO WA KUWA TAJIRI” wakati wa Ibada ya Sakramenti ya Kipaimara katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu John Mjini Bariadi, kilichoandikwa na Muumini wa Kanisa hilo Ndg.Vincent Mabula Jilala.
Mhashamu Askofu  wa Kanisa  Katoliki Jimbo la SHINYANGA Liberatus Sangu (katikati), Paroko wa Parokia ya Mtakatifu John Mjini Bariadi Padre Kizito(kulia) Nyanga na Mapadri wengine wakifuatilia Ujumbe wa Mkuu wa Mkoa wakati wa Ibada ya Sakramenti ya Kipaimara katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu John Mjini Bariadi.
Baadhi ya waumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu John wakiwa katikaIbada ya Sakramenti ya Kipaimara iliyoongozwa na Mhashamu Askofu  wa Kanisa  Katoliki Jimbo la SHINYANGA Liberatus Sangu (hayupo pichani)
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com