METDO Tanzania

METDO Tanzania

Saturday, August 5, 2017

Wakazi wa Mbagala kuanza kunufaika na Mradi wa Mabasi yaendayo Kasi baada ya Kimara na Mbezi

Mgeni rasmi wa Maadhimisho ya Sikukuu ya Wakulima Nane Nane Kitaifa Mkoani Lindi leo, Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi (KILIMO) Mhandisi Mathew Mtigumwe akimsikiliza Msemaji wa Mradi wa Mabasi yaendayo Kasi (DART) Bwana Mathew Kwembe. Mradi wa DART unatekelezwa chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu
Msemaji wa Mradi wa Mabasi yaendayo Kasi (DART) Bwana Mathew Kwembe akimweleza Mgeni rasmi wa Maadhimisho ya Sikukuu ya Wakulima Nane Nane Kitaifa Mkoani Lindi leo, Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi (KILIMO) Mhandisi Mathew Mtigumwe kuhusu ujenzi wa Barabara ya mwendokasi Awamu ya Pili ambayo itawahusu Wakazi wa Mbagala na Watumiaji wengine wa Barabara ya Kilwa
Mgeni rasmi wa Maadhimisho ya Sikukuu ya Wakulima Nane Nane Kitaifa Mkoani Lindi leo, Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi (KILIMO) Mhandisi Mathew Mtigumwe akipata maelezo katika Banda la Ofisi ya Waziri Mkuu, kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Nachingewa, Bibi Rukia Muwango
Wakazi wa Jiji la Dar es salam eneo la Mbagala na wale wanaotumia barabara ya Kilwa wanataraji kuanza kufurahia matunda ya huduma ya mabasi yaendayo kasi baada ya wale wa maeneo ya Kimara, Mbezi na maeneo mengine kuanza kufurahia huduma hiyo.

Afisa Habara wa Wakala wa Taifa wa Mradi wa Mabasi yaendayo Kasi, Bwana Mathew Kwembe kumwambia Mgeni rasmi wa Maadhimisho ya Sikukuu ya Wakulima Nane Nane leo, Mhandisi Mathew Mtigumwe ambaye ni Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Mifugona Uvuvi (KILIMO).

Bwana Kwembe amemwambia Mhandisi Mtigumwe kuwa ujenzi rasmi wa Barabara ya Kilwa kwa ajili ya kuwezesha mabasi yaendayo kasi kuanza kutumia barabara hiyo utaanza mapema Mwezi Februari mwaka 2018.

Aidha Bwana Kwembe ameongeza kuwa ujenzi huo wa Awamu ya Pili utaihusisha barabara ya Kilwa ambayo itajengwa kwa urefu wa Kilomita 19.3 ambapo ujenzi, utaanzia Mjini na kuishia eneo la Vikindu Jijini.

Bwana Kwembe amemwambia Mhandisi Mtigumwe kuwa baada ya ujenzi wa Barabara ya Kilwa kukamilika, itakuwa ni zamu ya wakazi wa Gongo la Mboto ambapo ujenzi utakuwa wa urefu wa Kilometa 23.6.

MWISHO
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com