Msemaji wa Mradi wa Mabasi yaendayo Kasi (DART) Bwana Mathew Kwembe akimweleza Mgeni rasmi wa Maadhimisho ya Sikukuu ya Wakulima Nane Nane Kitaifa Mkoani Lindi leo, Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi (KILIMO) Mhandisi Mathew Mtigumwe kuhusu ujenzi wa Barabara ya mwendokasi Awamu ya Pili ambayo itawahusu Wakazi wa Mbagala na Watumiaji wengine wa Barabara ya Kilwa
Mgeni rasmi wa Maadhimisho ya Sikukuu ya Wakulima Nane Nane Kitaifa Mkoani Lindi leo, Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi (KILIMO) Mhandisi Mathew Mtigumwe akipata maelezo katika Banda la Ofisi ya Waziri Mkuu, kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Nachingewa, Bibi Rukia Muwango
Wakazi wa Jiji la Dar
es salam eneo la Mbagala na wale wanaotumia barabara ya Kilwa wanataraji kuanza
kufurahia matunda ya huduma ya mabasi yaendayo kasi baada ya wale wa maeneo ya
Kimara, Mbezi na maeneo mengine kuanza kufurahia huduma hiyo.
Afisa Habara wa Wakala
wa Taifa wa Mradi wa Mabasi yaendayo Kasi, Bwana Mathew Kwembe kumwambia Mgeni
rasmi wa Maadhimisho ya Sikukuu ya Wakulima Nane Nane leo, Mhandisi Mathew
Mtigumwe ambaye ni Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Mifugona Uvuvi (KILIMO).
Bwana Kwembe amemwambia
Mhandisi Mtigumwe kuwa ujenzi rasmi wa Barabara ya Kilwa kwa ajili ya kuwezesha
mabasi yaendayo kasi kuanza kutumia barabara hiyo utaanza mapema Mwezi Februari
mwaka 2018.
Aidha Bwana Kwembe
ameongeza kuwa ujenzi huo wa Awamu ya Pili utaihusisha barabara ya Kilwa ambayo
itajengwa kwa urefu wa Kilomita 19.3 ambapo ujenzi, utaanzia Mjini na kuishia
eneo la Vikindu Jijini.
Bwana Kwembe amemwambia
Mhandisi Mtigumwe kuwa baada ya ujenzi wa Barabara ya Kilwa kukamilika, itakuwa
ni zamu ya wakazi wa Gongo la Mboto ambapo ujenzi utakuwa wa urefu wa Kilometa
23.6.
MWISHO
No comments:
Post a Comment