Baadhi ya mazao ya Misitu
zikiwemo mbao ambazo zitakuwa zikukusanywa kwa njia ya kielektroni
kupitia mfumo wa ukusanyaji maduhuli uliosanifiwa na Wizara ya Fedha na
Mipango unaoitwa Government Electronic Payment Gateaway-GEPG ikiwa ni
kutii agizo la Serikali ya awamu ya tano ya Rais John Magufuli ya
kuzitaka Taasisi za serikali kujiunga na mfumo huo.
Picha na Lusungu Helela
……………………….
Wakala wa Huduma za Misitu
Tanzania (TFS) imeanza utekelezaji wa ukusanyaji wa maduhuli kwa njia ya
kielektroniki kufuatia marekebisho ya sheria ya fedha ya mwaka 2017 na
maelekezo ya serikali ya awamu ya tano ambao umezitaka Taasisi za
serikali kujiunga na mfumo wa ukusanyaji maduhuli uliosanifiwa na Wizara
ya Fedha na Mipango unaoitwa Government electronic Payment
Gateaway-GEPG.
Akitoa ufafanuzi huo jana jijini
Dar es Salaam, Mhasibu Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania,
Peter Mwakosya amesema mashamba yote na ofisi za mameneja (DFM’s) wa
Taasisi hiyo zimeunganishwa katika mfumo huo.
Aidha amesema kutokana na
mazingira ya vizuia(Checkpoints) kutokidhi mahitaji ya mfumo huo na
hasa kushindwa kuhifadhi vitendea kazi kama kompyuta na printa kwa sasa
wakala inaendelea kuunganisha kwenye mfumo vizuia vyote kwa kutumia
vifaa maalum (Point of sales-POS).
Amebainisha kwamba vifaa hivyo
vitatumika kukusanya maduhuli na kuhakiki uhalali wa nyaraka
zinazokaguliwa katika vituo vyote vya ukaguzi wa mazao ya misitu na
nyuki kwa kipindi hiki ambacho vinaendelea kuunganishwa vizuia kwenye
mfumo wa moja kwa moja.
Mwakosya amesisitiza maduhuli
yote yatakayokusanywa kwenye vizuia yanawasilishwa Ofisi za mameneja wa
Misitu wa wilaya mapema ili yaingizwe kwenye mfumo.
Pia amewakumbusha wateja wote wa
Mazao ya Misitu na nyuki kuzingatia kwamba wanatakiwa kupata hati za
madai (Bill) katika mfumo kabla ya kwenda kufanya
Malipo.
Aidha, amewakumbusha wateja wa
bidhaa za Misitu na nyuki kwamba stakabadhi zilizokuwa zikitumika kabla
ya mfumo huo (ERV) hazitaendelea kutumika katika vituo vilivyounganishwa
na mfumo.
0 comments:
Post a Comment