Waziri wa Katiba na Sheria Prof
Palamagamba Kabudi (kushoto) akipokea moja ya Ripoti tatu alizokabidhiwa
na Katibu Mtendaji wa Tume ya Kurekebisha Sheria Casmir Kyuki, kushoto
ni Katibu wa Wizara ya Katiba na Sheria Prof Sifuni Mchome.
Waziri wa Katiba na Sheria Prof
Palamagamba Kabudi akizungumza na maofisa wa Tume na wale wa Wizara ya
Katiba na Sheria wakati wa makabidhiano ya Ripoti.
Katibu Mtendaji wa Tume ya
Kurekebisha Sheria Casmir Kyuki akizungumza wakati wa kukabidhi Ripoti
tatu kwa Waziri wa Katiba na Sheria Prof Palamagamba Kabudi.
Waziri wa Katiba na Sheria Prof
Palamagamba Kabudi akiangalia Ripoti alizokabidhiwa na Tume ya
Kurekebisha Sheria, wengine pichani ni Katibu wa Wizara ya Katiba na
Sheria Prof Sifuni Mchome (wa pili kushoto), Katibu Mtendaji wa Tume
Casmir Kyuki (kushoto kwa waziri), Katibu Msaidizi wa Tume Agnes
Mgeyekwa (Kulia) na Mkurugenzi Msaidizi Wizara ya Katiba na Sheria Mercy
Mrutu.
Prof Kabudi akiwa katika picha ya
pamoja na maofisa wa Wizara na wale wa Tume ya Kurekebisha Sheria wakati
wa tukio la kukabidhiwa Ripoti.
………………………
NA Munir Shemweta LRCT
Waziri wa Katiba na Sheria Prof.
Palamagamba Kabudi leo amepokea Ripoti tatu zilizofanyiwa kazi na Tume
ya Kurekebisha Sheria Tanzania.
Ripoti alizokabidhiwa Prof.
Kabudi ni Mapitio ya Mfumo wa Sheria Unaosimamia Usajili wa Matukio
Muhimu ya Binadamu na Takwimu, Mfumo wa Sheria Zinazosimamia Huduma za
Jamii kwa Wazee na Ripoti ya Mapitio ya Mfumo wa Sheria Zinazohusu Haki
za Walaji na Watumiaji Bidhaa na Huduma.
Mkabidhiano ya ripoti hizo
yamefanyika leo baina ya Waziri wa Katiba na Sheria na Katibu Mtendaji
wa Tume ya Kurekebisha Sheria Casmir Kyuki jijini Dar es Salaam.
Akizungumza wakati wa makabidhiano
ya ripoti hizo Prof. Kabudi ameipongeza Tume ya Kurekebisha Sheria
Tanzania kwa kazi nzuri iliyoifanya ya kufanya mapitio na hatimaye kuja
na mapendekezo yanye lengo la kuboresha sheria husika.
Amesema, Tume ni taasisi muhimu
sana katika kufanya mapito ya sheria mbalimbali na kuweka bayana kuwa,
kuna haja ya mapitio ya sheria mbalimbali yanayofanyika nchini
kuishirikisha Tume ambayo ina jukumu la kufanya hivyo kulingana na
sheria iliyoianzisha.
Akielezea Mapitio ya Sheria
inayosimamia Usajili wa Matukio Muhimu ya Binadamu na Takwimu Prof.
Kabudi amesema kutokana na umuhimu wa sheria hiyo atahakikisha
mapendekezo ya sheria hiyo yanafanyiwa kazi haraka ikiwa ni pamoja na
kuwasilishwa katika kikao kijacho cha Bunge la mwezi Septemba.
Kuhusu Sheria ya Huduma za Jamii
kwa Wazee, Waziri wa Katiba na Sheria ameieleza ripoti hiyo kuwa ni
muhimu sana hasa ikizingatiwa wazee wanakabiliwa na changamoto
mbalimbali kama vile huduma za afya na pensheni na kusisitiza kuwa kila
mtu ni mzee mtarajiwa.
Aidha, Prof Kabudi amezitaka
Taasisi zote zilizo chini ya wizara ya Katiba na Sheria kushirikiana
katika kazi zake hususan katika mapitio ya sheria mbalimbali ili kuja
matokeo chanya katika sekta ya sheria.
Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa
Tume ya Kurekebisha Sheria anzania Bw. Casmir Kyuki alisema Tume yake
imefanya utafiti wa kina wakati wa kupitia sheria hizo tatu ikiwa ni
pamoja kutembelea maeneo mbalimbali nchini lengo likiwa ni kupata maoni
kutoka kwa wadau ambao ni taasisi za serikali, mashirika yasiyo ya
kiserikali na wananchi wa kawaida.
Munir Shemweta
Afisa Habari
0655 959465/0786249844
11 Agosti, 2011
0 comments:
Post a Comment