Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini,
IGP Simon Sirro akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Operesheni Maalumu za
Jeshi la Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Liberatus Sabas
kuhusiana na tukio la kuuawa wahalifu 13 katika majibizano ya risasi
baina ya Polisi na wahalifu hao katika eneo la Tangibovu, Kijiji cha
Miwaleni Kata ya Mchukwi, Tarafaya Kibiti.Chini ni silaha 8 aina ya SMG
pamoja na vifaa vingine zilizopatikana katika majibizano hayo.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini,
IGP Simon Sirro akionesha makasha ya risasi(magazine) ambazo ni miongoni
mwa makasha 8 yaliyokuwa ya kitumiwa na wahalifu katika eneo la
Tangibovu, Kijiji cha Miwaleni Kata ya Mchukwi, Tarafa ya Kibiti. Wa
kwanza kushoto ni Kamishina wa Polisi Jamii (CP) MussaAlli Musa
akifuatiwa na Mkuu wa Operesheni Maalumu za Jeshi la Polisi,Naibu
Kamishna wa Polisi (DCP) Liberatus Sabas. Katikat ukio hilo Jeshi la
Polisi limefanikiwa kuwaua wahalifu 13 ambao walikuwa wakifanya mauaji
Kibiti.
Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro akielezea baadhi ya vitu
mbalimbali vilivyokuwa vikitumiwa na wahalifu 13 walioua wakatika eneo
la Tangi bovu, Kijiji cha Miwaleni Kata ya Mchukwi, Tarafa ya Kibiti
ambapo jumla ya silaha 8 ainaya SMG, risasi 158,pikipiki 2, pamoja na
begi la nguo vilivyokuwa vikitumiwa na wahalifu hao. Kushoto ni
Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya jinai (CP) Robert Boaz
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini,
IGP Simon Sirro akionesha silaha aina ya SMG ambayo ni miongoni mwa
silaha 8 zilizokuwa zikitumiwa na wahalifu 13 walioua wakatika
majibizano ya risasi baina yao na Jeshi la Polisi katika eneo laTangi
bovu, Kijiji cha Miwaleni Kata ya Mchukwi, Tarafa ya Kibiti.Wa kwanza
kulia ni Kamishina wa Polisi Jamii (CP) Mussa Alli Musa akifuatiwa na
Mkuu wa Operesheni Maalumu za Jeshi la Polisi,Naibu Kamishna wa Polisi
(DCP) Liberatus Sabas.–
Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro akiongea na wananchi wa
Kijiji cha Miwaleni Kata ya Mchukwi, Tarafa ya Kibiti alipokuwa akitoka
kukagua eneo la tukio walipouawa wahalifu 13 katika majibizano ya risasi
baina yao na Jeshi la Polisi katika eneo la Tangi bovu. –
Picha na Jeshi La Polisi
0 comments:
Post a Comment