METDO Tanzania

METDO Tanzania

Thursday, August 10, 2017

WHC YAFUNGUA DIRISHA LA UUZAJI WA NYUMBA KWA WATUMISHI WA MASHIRIKA BINAFSI NA WACHANGIAJI WA HIARI, MUHIMU UWE MWANACHAMA WA MIFUKO YA JAMII

1
Mkurugenzi Mkuu wa Watumishi Housing Limited (WHC) Dk. Freddy Msemwa akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za shirika hilo jijini Dar es salaam wakati alipotangaza mpango mpya wa shirika hilo ambapo linaanza kuuza nyumba kwa wafanyakazi wa Mashiriki Binafsi na wachangiaji Binafsi waliojiunga katika mifuko ya jamii ambapo amesema tayari utaratibu huo umeshaanza na mtu yeyote ambaye ni mwanachama katika mifuko ya Jamii na ni mtumishi wa Serikali au mashirika binafsi au mchangiaji binafsi anaruhusiwa kununua nyumba katika shirika hilo kama mnununzi mpangaji wa shirika hilo na baada ya miaka 25 akimaliza deni lake au akimaliza kabla ya muda huo atakabidhiwa hati ya umiliki wa nyumba hiyo na kuwa mmiliki kamili, Katika Picha kushoto ni Bw. Raphael Mwabuponde Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mauzo (WHC)
2
Mkurugenzi Mkuu wa Watumishi Housing Limited (WHC) Dk. Freddy Msemwa akimsikiliza Bw. Raphael Mwabuponde Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mauzo (WHC) wakati alipokuwa akifafanua jambo kwa waandishi wa habari katika mkutano huo kulia ni Maryjane Makawia Afisa Mauzo na Mwasiliano (WHC)
3
Mkurugenzi Mkuu wa Watumishi Housing Limited (WHC) Dk. Freddy Msemwa akieleza jambo katika mkutano huo kwa jinsi shirika hilo lilivyojizatiti katika uuzaji wa nyumba zinazojengwa katika miradi yake hapa nchini , kulia ni Maryjane Makawia Afisa Mauzo na Mwasiliano (WHC) na kushoto ni Bw. Raphael Mwabuponde Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mauzo (WHC) 
4
Mkurugenzi Mkuu wa Watumishi Housing Limited (WHC) Dk. Freddy Msemwa na Bw. Raphael Mwabuponde Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mauzo (WHC)wakimsikiliza Irene Kasanda Afisa Mauzo wa (WHC) wakati akielezea namna wana Diaspora wanavyoweza kunufaika na mpango huo.
5
Mkurugenzi Mkuu wa Watumishi Housing Limited (WHC) Dk. Freddy Msemwa sisitiza jambo wakati alipokuwa akifafanua mambo mbalimbali kwa waandishi wa habari kulia ni Maryjane Makawia Afisa Mauzo na Mwasiliano (WHC).

Watumishi Housing Company (WHC) ni mfuko wa uwekezaji wa pamoja ulio anzishwa kwa lengo la kujenga na kuuza nyumba za bei nafuu kwa Watumishi wa umma kwa mikopo nafuu ya muda mrefu.
Watumishi Housing Company (WHC) inapenda kuijulisha umma kwamba imefungua dirisha kwaajili ya kuuza nyumba zake kwa wafanyakazi wote. Hii inajumuisha wafanyakazi walio katika utumishi wa umma na wale ambao hawako katika utumishi wa umma lakini wanachangia katika mifuko ya pensheni. Wigo huu mdogo unakuja baada ya kuonekana watu wengi ukitoa watumishi wa umma wana shida ya makazi bora na ya kisasa ni wachangiaji katika mifuko ya pensheni ambayo ndiyo wamiliki wa Watumishi Housing, hivyo basi taasisi ikaona itoe nafasi kwa wachangiaji wengine wa mifuko ya pensheni kuweza kupata nyumba za kisasa, bora na za bei nafuu.

Kufuatia uamuzi huu, Watumish Hosing Company sasa itakua ikiwahudumia watumishi wa umma pamoja na wafanyakazi wengine walioko katika sekta binafsi. Uamuzi huu ni muendelezo wa juhudi za serikali na mifuko ya hifadhi ya jamii katika kuwawezesha wafanyakazi wote kuwa na makazi bora na kuwawezesha kiuchumi kupitia umiliki wa nyumba.

Watumishi Housing inapenda kuwakaribisha watanzania wote kwa ujumla kutuma maombi yao ya nyumba kwa kuchukua fomu katika tovuti ya www.whctz.org au kwa kufika katika ofisi zilipo jengo la Golden Jubilee Towers ghorofa ya 4. Kwasasa tuna nyumba za kuuza zilizopo Bunju B, Gezaulole Kigamboni, Mkundi Morogoro, Mwanza Kisesa na Njedengwa Dodoma. Vilevile tunapenda kusisitiza kwamba watumishi wa umma watapewa kipaumbele katika kupata nyumba kwani wao ndio kipaumbele cha taasisi.

Watumishi Housing Company (WHC) ni mfuko wa uwekezaji wa pamoja wenye jukumu la kujenga nyumba za gharama nafuu kwa ajili ya watumishi wa umma. Jukumu lingine la WHC ni kusimamia dhamana ya uwekezaji nyumba (Real estate investment Trust- REIT) kupitia uwekezaji katika vipande. WHC inamilikiwa na mifuko ya hifadhi ya jamii lakini baada ya muda si mrefu WHC itaweza kumilikiwa na kila mtanzania kupitia uwekezaji wa vipande.

Watumishi Housing tunashauri watumishi kununua nyumba tayari zilizojengwa na zilizo bora na za kisasa badala ya kununua ardhi na kuanza ujenzi. Kwakufanya hivi utakua unanunua nyumba ambayo tayari imeishajengwa kwa ubora na kisasa kwa bei nafuu kabisa vilevile utakua unaondokana na matatizo mengi sana yanayokuja na ujenzi kama kupoteza muda, gharama kubwa
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com