Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa. Makame Mbarawa akipanda juu ya Barabara ya Juu
(Tazara Flyover) inayoendelea kujengwa katika eneo la Tazara Jijini Dar
es Salaam wakati wa Ziara ya Rais wa Shirika la Maendeleo Kimataifa la
Japan (JICA Dkt. Shinichi Kitaoka aliyewasili nchini.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa. Makame Mbarawa akimuelezea jambo Rais wa Shirika
la Maendeleo Kimataifa la Japan (JICA) Dkt. Shinichi Kitaoka (kushoto)
alipotembelea kukagua maendeleo ujenzi wa Barabara ya Juu (Tazara
Flyover) inayoendelea kujengwa katika eneo la Tazara Jijini Dar es
Salaam.
Rais wa Shirika la Maendeleo Kimataifa
la Japan (JICA) Dkt. Shinichi Kitaoka akimuelezea jambo Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kulia)
alipotembelea kukagua maendeleo ujenzi wa Barabara ya Juu (Tazara
Flyover) inayoendelea kujengwa katika eneo la Tazara Jijini Dar es
Salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa. Makame Mbarawa akisikiliza maelezo kutoka kwa mmoja
wa wataalamu wa Kampuni ya Ujenzi ya Sumitomo Mitsui wakati wa ziara
ya Rais wa Shirika la Maendeleo Kimataifa la Japan (JICA) Dkt. Shinichi
Kitaoka (watatu kushoto) alipotembelea kukagua maendeleo ujenzi wa
Barabara ya Juu (Tazara Flyover) inayoendelea kujengwa katika eneo la
Tazara Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa. Makame Mbarawa akitazama mchoro wa mradi wa ujenzi
wa Barabara ya Juu (Tazara Flyover) wakati wa ziara ya Rais wa Shirika
la Maendeleo Kimataifa la Japan (JICA) Dkt. Shinichi Kitaoka (kushoto
kwake) alipotembelea kukagua maendeleo ya ujenzi wa Barabara hiyo
Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni mmoja wa wataalamu wa Kampuni ya
Ujenzi ya Sumitomo Mitsui ambayo ndiyo mkandarasi wa mradi huo
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa na Rais wa Shirika la Maendeleo
Kimataifa la Japan (JICA) Dkt. Shinichi Kitaoka wakiwa katika picha ya
pamoja na baadhi ya watendaji wa TANROADS, na wataalamu wa Ujenzi mara
baada ya kumaliza ziara ya kukagua maendeleo ujenzi wa Barabara ya Juu
(Tazara Flyover) inayoendelea kujengwa katika eneo la Tazara Jijini Dar
es Salaam.
Muonekano wa Juu na Pembeni mwa bararaba
ya Juu (Tazara Flyover) ambao ujenzi wake umekamiklika kwa asilimia 53
na unatarajiwa kukamilika mapema mwezi wa kumi mwakani.
Picha na: Idara ya Habari – MAELEZO
0 comments:
Post a Comment