Ofisi
ya Bunge Leo imeeleza kuwa Spika Job Ndugai amepokea barua kutoka kwa
Maalif Seif Sharif Hamad yenye maelezo ya kuwafuta uanachama wabunge
wawili Magdalena Hamis Sakaya na Maftaha Abdallah Nachuma akidai wamekosa sifa ya kuendelea na Ubunge.
Taarifa
ya ofisi ya Bunge imeeleza kuwa ofisi ya Spika inayo barua ya
Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha CUF Prof. Ibrahim Lipumba yenye
kumbukunbu namba CUF/AK/DSM/MKT/05/2017 ya March 22, 2017 ikiliarifu
Bunge kuwa Maalim Seif ameshindwa kutekeleza majukumu yake kama Katibu
Mkuu hivyo kwa mujibu wa Katiba ya CUF, majukumu ya Katibu Mkuu
yatatekelezwa kuanzia tarehe hiyo na Magdalena Sakaya.
==>Soma barua nzima hapo chini
0 comments:
Post a Comment