Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu imetupilia mbali maombi ya Wema Sepetu ya kutaka
kielelezo cha sampuli ya mkojo wake kisipokelewe mahakamani.
Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba amesema anakubaliana na upande wa mashtaka kwamba kielelezo cha mkojo wa Wema kipokelewe na Mahakama kama sehemu ya ushahidi.
Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba amesema anakubaliana na upande wa mashtaka kwamba kielelezo cha mkojo wa Wema kipokelewe na Mahakama kama sehemu ya ushahidi.
Pingamizi
la Wema kupitia wakili wake Kibatala ni kwamba ripoti iliyowasilishwa
na Mkemia kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu, Elias Mlima ya kwamba mkojo wa
Wema una chembe chembe za dawa za kulevya aina ya Bangi haikukidhi
matakwa ya kisheria. Kutokana na hatua hiyo, Hakimu Simba ameahirisha
kesi hiyo hadi Agosti 16/2017.
Wema Sepetu na wengine wawili wanakabiliwa na makosa ya kukutwa na dawa za kulevya aina ya bangi Februari mwaka huu .
0 comments:
Post a Comment