METDO Tanzania

METDO Tanzania

Sunday, August 20, 2017

SHAKA: MANTIKI NA DHANA YA KUWEPO UPINZANI NCHINI IMEPOTEA

ALICHOKISEMA KAIMU KATIBU MKUU UVCCM TAIFA SHAKA HAMDU SHAKA (MNEC) KUHUSU UZALENDO NA UNAFIKI WA WANASIASA  KUTAKA KULIFITINISHA TAIFA 19/08/2017.

"Msingi, mantiki na dhana ya kuwepo upinzani imepotea nchini  na sasa vyama vya upinzani hususan Chadema kImejikita katika siasa chafu za kupandikiza chuki na uchochezi wenye malengo hatarishi kwa Taifa."- Shaka

" Ushindani wa hoja kwa hoja umeachwa na kuwashinda wapinzani  badala yake wamehamia kukaanga mbuyu kwa dhumuni la kuigombanisha serikali ili  ichukiwe na wananchi."- Shaka

"Katika masuala ya utawala jambo la uingiaji mikataba au kuvunjwa ni mambo yanayojitokeza hivyo haiwezi kuwa ndiyo hoja ya msingi kwa mwanasiasa na chama chake kupoteza muda na kuropoka hovyo mbele ya jamii." Shaka

"Hata Waziri Mkuu mstaafu ambaye ni Mwenyekiti wa kanda ya Pwani Chadema Fredrick Sumaye aliwahi kuvunja halmashauri ya jiji la Dar Es  Salama na madiwani wakapoteza nafasi zao."-Shaka 

" Bila shaka alitimiza wajibu huo kwa kutazama maslahi mapana ya maendeleo ya jiji la Dar es Salaam na ufanisi  wake kwa ujumla." -Shaka

"Waziri Mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa ya Richmond Edward Lowassa aliwahi kuvunja mkataba kati ya serikali na kampuni ya "City Water" jambo ambalo pia linaweza kuwa na mtazamo wa kulinda maslahi ya umma" - Shaka

"Mungu ampe upeo Tundu Lisu hajui masuala ya utawala katika medani za kidola kwa vile ni mwanasiasa mwanagenzi asiye na uzoefu wa kutosha na ni  mtu wa kukurupuka, kama hoja  ni kudaiwa,  Serikali zote  duniani, taasisi za kibenki, mashirika ya kimataifa pia hudaiwa, hakuna asiyedaiwa " -Shaka. 

"Waziri dhamana au kiongozi yoyote mwandamizi  wa serikali hawezi kuamka nyumbani wake akavunja mkataba iwapo mambo hayaendi kama ilivyokusudiwa bila kupata idhini ya mamlaka za nchi zinazohusika kama anaavyofikiri Lisu na wenzake." - Shaka

"Lisu anafanya uchochezi wa kisiasa ili kujitafutia umaarufu kwa masuala ambayo hayamsaidii yeye wala Chadema na washirika wao wanadhani wanapambana na mtu. Mbona hakuhoji Sumaye na Lowasa jinsi walivyoshiriki kuvunja mikataba. Asitegemee  kupata sifa kwa kujionyesha kwake kuwa si  mzalendo halisi kwa taifa " - Shaka 

"Awali kulikuwa na wanasiasa wa  upinzani uliojiegemeza katika mambo ya msingi ya kuhimiza misingi  ya utawala bora, uwajibikaji, nidhamu ya kazi na kutaka ziwepo juhudi za kukomesha rushwa." - Shaka

 "Kuna wakati fulani upinzani uliitaka serikali kushughulikia mikataba ya madini, kudhibiti wizi wa mali za umma, kukomesha uzembe kazini na kupambana na ujambazi masuala ambayo sasa yametekelezwa kwa ufanisi mkubwa na Rais Magufuli." - Shaka

"Lisu na Chadema baada ya kuona yupo Rais anayesimamia mambo ya utawala na uongozi wa nchi kwa umakini na uhalisia, wameacha kazi ya upinzani sasa wameamua kufanya ufutini na  uchochezi lazima afahamu kuwa uchochezi ni gharama, usipodhibitiwa nchi itayumba "- Shaka

" Wananchi wazipuuze hekaya na porojo za kina Lisu na Chadema kwa maelezo kuwa  chama hicho kimefilisika na kwa bahati mbaya  kina upungufu wa namba ya wanasiasa wenye upeo, maarifa ya kisiasa na wanaothamini utaifa na uzalendo"- Shaka

"Kama kuna jambo lolote linalogusa maslahi ya Taifa tuendelee kuwaamini  viongozi wetu litashuhulikiwa kwa mujibu  wa katiba na sheria. Hakuna mafanikio yasiyo na changamoto na hakuna changamoto zisizo mafanikio siku zote ni vitu vinavyojitegemeana." - Shaka

"UVCCM rai yetu kwa Watanzania kuendelea  kumuombea na kumtia  nguvu  Rais wetu Dk John Pombe Magufuli anapita katika wimbi zito lakini tunaamini atatuvusha  salama na kwa mafanikio makubwa." -Shaka

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com