ALICHOKISEMA KAIMU KATIBU MKUU UVCCM TAIFA SHAKA HAMDU SHAKA (MNEC) KUHUSU UZALENDO NA UNAFIKI WA WANASIASA KUTAKA KULIFITINISHA TAIFA 19/08/2017.
"Msingi, mantiki na dhana ya kuwepo upinzani imepotea nchini na sasa vyama vya upinzani hususan Chadema kImejikita katika siasa chafu za kupandikiza chuki na uchochezi wenye malengo hatarishi kwa Taifa."- Shaka
" Ushindani wa hoja kwa hoja umeachwa na kuwashinda wapinzani badala yake wamehamia kukaanga mbuyu kwa dhumuni la kuigombanisha serikali ili ichukiwe na wananchi."- Shaka
"Katika masuala ya utawala jambo la uingiaji mikataba au kuvunjwa ni mambo yanayojitokeza hivyo haiwezi kuwa ndiyo hoja ya msingi kwa mwanasiasa na chama chake kupoteza muda na kuropoka hovyo mbele ya jamii." Shaka
"Hata Waziri Mkuu mstaafu ambaye ni Mwenyekiti wa kanda ya Pwani Chadema Fredrick Sumaye aliwahi kuvunja halmashauri ya jiji la Dar Es Salama na madiwani wakapoteza nafasi zao."-Shaka
" Bila shaka alitimiza wajibu huo kwa kutazama maslahi mapana ya maendeleo ya jiji la Dar es Salaam na ufanisi wake kwa ujumla." -Shaka
"Waziri Mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa ya Richmond Edward Lowassa aliwahi kuvunja mkataba kati ya serikali na kampuni ya "City Water" jambo ambalo pia linaweza kuwa na mtazamo wa kulinda maslahi ya umma" - Shaka
"Mungu ampe upeo Tundu Lisu hajui masuala ya utawala katika medani za kidola kwa vile ni mwanasiasa mwanagenzi asiye na uzoefu wa kutosha na ni mtu wa kukurupuka, kama hoja ni kudaiwa, Serikali zote duniani, taasisi za kibenki, mashirika ya kimataifa pia hudaiwa, hakuna asiyedaiwa " -Shaka.
"Waziri dhamana au kiongozi yoyote mwandamizi wa serikali hawezi kuamka nyumbani wake akavunja mkataba iwapo mambo hayaendi kama ilivyokusudiwa bila kupata idhini ya mamlaka za nchi zinazohusika kama anaavyofikiri Lisu na wenzake." - Shaka
"Lisu anafanya uchochezi wa kisiasa ili kujitafutia umaarufu kwa masuala ambayo hayamsaidii yeye wala Chadema na washirika wao wanadhani wanapambana na mtu. Mbona hakuhoji Sumaye na Lowasa jinsi walivyoshiriki kuvunja mikataba. Asitegemee kupata sifa kwa kujionyesha kwake kuwa si mzalendo halisi kwa taifa " - Shaka
"Awali kulikuwa na wanasiasa wa upinzani uliojiegemeza katika mambo ya msingi ya kuhimiza misingi ya utawala bora, uwajibikaji, nidhamu ya kazi na kutaka ziwepo juhudi za kukomesha rushwa." - Shaka
"Kuna wakati fulani upinzani uliitaka serikali kushughulikia mikataba ya madini, kudhibiti wizi wa mali za umma, kukomesha uzembe kazini na kupambana na ujambazi masuala ambayo sasa yametekelezwa kwa ufanisi mkubwa na Rais Magufuli." - Shaka
"Lisu na Chadema baada ya kuona yupo Rais anayesimamia mambo ya utawala na uongozi wa nchi kwa umakini na uhalisia, wameacha kazi ya upinzani sasa wameamua kufanya ufutini na uchochezi lazima afahamu kuwa uchochezi ni gharama, usipodhibitiwa nchi itayumba "- Shaka
" Wananchi wazipuuze hekaya na porojo za kina Lisu na Chadema kwa maelezo kuwa chama hicho kimefilisika na kwa bahati mbaya kina upungufu wa namba ya wanasiasa wenye upeo, maarifa ya kisiasa na wanaothamini utaifa na uzalendo"- Shaka
"Kama kuna jambo lolote linalogusa maslahi ya Taifa tuendelee kuwaamini viongozi wetu litashuhulikiwa kwa mujibu wa katiba na sheria. Hakuna mafanikio yasiyo na changamoto na hakuna changamoto zisizo mafanikio siku zote ni vitu vinavyojitegemeana." - Shaka
"UVCCM rai yetu kwa Watanzania kuendelea kumuombea na kumtia nguvu Rais wetu Dk John Pombe Magufuli anapita katika wimbi zito lakini tunaamini atatuvusha salama na kwa mafanikio makubwa." -Shaka
No comments:
Post a Comment