METDO Tanzania

METDO Tanzania

Sunday, August 13, 2017

RAIS MSTAAFU AWAMU YA PILI ALI HASSAN MWINYI AWAASA MADEREVA KUZINGATIA SHERIA ZA BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI

PIX 1
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi, akisikiliza maelezo kutoka kwa Inspekta Ibrahim Samwix, wakati alipotembelea mabanda mbalimbali kwenye Tamasha la Usalama Barabarani lililofanyika Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
PIX 2
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi (aliyevaa suti), akisikiliza maelezo jinsi uvunjaji wa sheria za usalama barabarani unavyoweza kusababisha ajali, wakati alipotembelea banda la Maaskari wa usalama barabarani, kwenye Tamasha la Usalama Barabarani lililofanyika jana Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
PIX 3
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto), akimkabidhi tuzo Mgeni Rasmi, Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi, wakati wa Tamasha la Usalama Barabarani lililofanyika jana Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
PIX 4
Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Nsato Marijani (kushoto), akipokea zawadi kutoka kwa  Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni kwa  niaba ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro kwa kutambua mchango wake katika suala nzima la Usalama Barabarani wakati wa Tamasha la Usalama Barabarani lililofanyika jana, Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.Kulia ni Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
PIX 5
Balozi wa Usalama Barabarani, Samira Abuu (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na Mgeni Rasmi, Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi na Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani,Mhandisi Hamad Masauni, baada ya kupokea cheti cha kutambua mchango wake katika masuala ya Usalama Barabarani wakati wa Tamasha la Usalama  Barabarani lililofanyika jana, Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com