Na Dotto Mwaibale, Masasi
WANANCHI
wa Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara wamelilamikia Shirika la Umeme
Tanzania (TANESCO) kutokana na kuwakatia umeme mara kwa mara na
kusabisha kuwaunguzia vifaa vyao vya majumbani na kuwa hadha kwao.
Wakizungumza
na waandishi wa habari wilayani hapa leoa wananchi hao walisema kuwa
tabia hiyo ya kukatiwa umeme mara kwa mara imekuwa sugu na hawajui kilio
chao hicho wakipeleke wapi.
”
Hii tabia ya kukatiwa umeme kila siku tena bila ya kupewa taarifa
imekuwa sugu hapa wilayani kwetu hatuji ni nani tumuambie” alisema
Muharami Hamisi mkazi wa mjini hapa.
Hamisi
alisema wananchi wengi wamekuwa wakiunguliwa vifaa vyao vinavyotumia
umeme zikiwemo taa lakini wanakaa kimya kwa kuwa hajui wapi waende
kulalamika.
Mwajabu
Liganga alisema wanaona kama Tanesco wanawafanyia makusudi kuhusu
kukatika huko kwa umeme kwa mara kwa mara kwani wanapofika viongozi wa
kitaifa katika mji huo huwa hawakati umeme unawashwa kuanzia asubuhi
hadi jioni.
“Tunashangaa
wanapofika viongozi wa kitaifa hapa wilayani umeme haukatwi lakini
wakiondoka tu hali inarudi palepale” alisema Liganga.
Liganga
aliongeza kuwa umeme huo kwa siku umekuwa ukikatwa na kuwashwa kwa
zaidi ya mara kumi bila ya kuwepo kwa maelezo ya kina.
Akizunguzia
madai hayo Ofisa Usambaji wa Umeme wa Wilaya hiyo aliyetajwa kwa jina
la Iddi Kuhanga alikiri kuwepo kwa changamoto hiyo akieleza kuwa sababu
kubwa ni uwezo wa uzalishaji wa umeme huo kuwa mdogo.
Alisema
kuwa umeme unaotumika wilayani hapo unatoka mkoani Mtwara hivyo hadi
ufike Masasi unakumbana na changamoto nyingi ikiwemo ya kuharibiwa kwa
miundombinu kwa kuangukiwa na miti kutokana na shughuli za kilimo au
ndege kukaa kwenye nyaya.
Kuhanga alikanusha madai ya kuwa wanapofika viongozi wa kitaifa hali hiyo ya kukatika umeme huo inakuwa haipo.
0 comments:
Post a Comment