Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakar
Zubeir akiwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
Mheshimiwa William Lukuvi akimsisitiza kufuatilia kwa makini maeneo yote
ya waislam yanayomilikiwa na BAKWATA na yaliyomilikishwa watu kinyume
cha utaratibu yanatafutiwa ufumbuzi kama alivyoagiza Mheshimiwa Rais.
Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakar
Zubeir akimkabidhi Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
Mheshimiwa William Lukuvi Ripoti ya Tume ya Mufti ofisini kwa Waziri.
Ujumbe wa Tume ya Mufti ukiwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi ofisini kwake.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi akimsikiliza Mufti wa
Tanzania Sheikh Abubakar Zubeir mara baada ya kupokea Ripoti ya Tume ya
Mufti ofisini kwake, kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu wa BAKWATA Mwalimu
Salim Abeid na Mjumbe wa Baraza la Ulamaa Sheikh Ally Ngeruko.
Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakar
Zubeir akiwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
Mheshimiwa William Lukuvi baada ya kumkabidhi Ripoti ya Tume ya Mufti.
……………………….
Waziri wa Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi amekutana na Mufti Sheikh
Abubakar Zubeir pamoja ujumbe wake wa Tume ya Mufti iliyoundwa
kuhakikisha kwamba mali za waislam zinazomilikiwa na BAKWATA zinar
ejeshwa.
Waziri Lukuvi amepokea ripoti hiyo
ikiwa ni kutekeleza agizo la Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli la
kumtaka Waziri Ardhi afuatilie kwa makini maeneo yote ya waislam
yanayomilikiwa na BAKWATA na yaliyomilikiswa watu kinyume cha utaratibu
yanatafutiwa ufumbuzi.
Katika ujumbe huu Mufti
ameongozana na Kaimu Katibu Mkuu wa BAKWATA Mwalimu Salim Abeid, Mjumbe
wa Baraza la Ulamaa Sheikh Ally Ngeruko, Makamu mwenyekiti wa Tume ya
Mufti na Mjumbe wa Baraza la Ulamaa Sheikh Issa Othman Issa na Katibu wa
Tume ya Mufti Alhaj Omary Igge.
Baada ya kukabithi ripoti hii
Mufti Sheikh Abubakar Zubeir amemshukuru Waziri wa Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi kwa kupokea Ujumbe wake wa
Tume ya Mufti na kumuomba achunguze na kuchambua kwa makini maeneo yote
ya Bakwata yanayohusiana na migogoro ya ardhi.
Tume hii ya Mufti ya Kuhusu
urejeshaji wa mali za waislam iliundwa na Mufti Sheikh Abubakar Zubeir
mara baada ya kukukutana Mheshimiwa Rais na kumuomba awasaidie
kuhakikisha kwamba mali za waislam zinazomilikiwa na BAKWATA
zinarejeshwa BAKWATA.
Mara baada ya kupokea ripoti hii
Waziri Lukuvi amemuahidi Mufti Sheikh Abubakar Zubeir kwamba atatekeleza
agizo hilo la Mheshimiwa Rais na ataifanya kazi hii katika muda mfupi
ujao na kusimamia kikamilifu kwa kufuata sheria.
0 comments:
Post a Comment