Serikali mkoani Kigoma Imetakiwa kuanza miradi ya ujenzi wa Zahanati katika kila kijiji na Vituo vya afya kwenye kila kata sambamba na kukamilisha majengo yaliyojenga na wananchi.
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
watoto Daktari Hamis Kigwangala ameyasema hayo hivi karibuni Katika
kijiji cha Mwakizega Kata ya Mwakizega Wialaya ya Uvinza mkoani hapa,
wakati akifungua mradi wa majengo 26 ya kutolea huduma za afya ya mama
na mtoto majengo yanayojengwa kwa udhamini wa shirika la Ingender
Hearth.
Amesema licha ya kujengewa vituo 26 katika vijiji tofauti
mkoani hapa lakini bado kuna uhitaji wa vituo vya afya na zahanati
kutokana na mahitaji ya wananchi waishio vijijini, na amewataka
viongozi kutoa ushirikiano kwa wananchi pale wanapoanza kujengo vituo
hivyo.
Aidha kwa Upande wake Mkuu wa mkoa wa Kigoma Brigedia
General Mstaafu Emmanuel Maganga amesema mkoa umepiga hatua kutokana na
msaada wa majengo hayo 26 yatakayotoa huduma za afya na sambamba na
kuahidi kuyatumia majengo hayo kwa manufaa ya wananchi na amewataka
wananchi kuyatunza kwa ajiri ya manufaa ya afya zao.
Kwa Upande wake Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa Daktari Fadhiri
Kibaya, amesema mkoa una jumla ya Vituo vya kutolea huduma za afya 278
huku mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi MAM ni kuwa na Zahanati
katika kila kijiji na Kituo cha afya kwa kila kata huku akibainisha kuwa
changamoto inayoikabiri sekta ya Afya mkoani hapa ni Kukosekana kwa
watumishi pia bado kuna uhitaji wa zahanati na vituo vya afya.
Nae Mkurugenzi wa Shirika la Engender Hearth Tanzania Lulu
Ngwanakilala amesema shirika hilo limeweka kipaumbele katika kuleta
mabadiriko ya kudumu hususa ni katika afya ya jamii huku akibainisha
kuwa gharama iliyotumika katika ujenzi wa majengo hayo ni shilingi
bilioni 2.75.
0 comments:
Post a Comment