METDO Tanzania

METDO Tanzania

Sunday, August 20, 2017

Rais Buhari arejea nyumbani baada ya siku zaidi ya 100 London

media
Rais Muhammadu Buhari na makamu wake Yemi Osinbajo katika uwanja wa ndege wa Abuja, 19 08 2017.
Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari, jana Jumamosi amerejea nyumbani akitokea London Uingereza alikokuwa akipatiwa matibabu kwa takribani miezi mitatu.

Buhari amepokelewa na Wafuasi wake waliojipanga katika barabara za mji mkuu wakiimba na kucheza, ambapo maafisa wa ngazi za juu serikalini akiwemo makamu wake nao walikusanyika kumkaribisha Buhari.

Buhari mwenye umri wa miaka 74 aliondoka nchini mwake mnamo Mei 7 ambapo kutokurejea kwake kwa muda mrefu kulisababisha mvutano ambapo wananchi waliandamana na kutoa wito kumtaka arejee nyumbani au ajiuzulu.

Taarifa ya ikulu imeeleza kuwa rais Buhari, atalihutubia taifa Kesho Jumatatu.

Chanzo:RFI
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com