METDO Tanzania

METDO Tanzania

Sunday, March 6, 2016

PRF MBARAWA MGENI RASMI TAMASHA LA PASAKA KAHAMA

mba

NA MWANDISHI WETU

WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa anatarajia kuwa mgeni rasmi kwenye Tamasha la Pasaka linalotarajia kufanyika Machi 28 kwenye uwanja wa Taifa mjini Kahama.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya Tamasha la Pasaka, Alex Msama Profesa Mbarawa amekubali kuwa mgeni rasmi katika tamasha hilo ambalo linashirikisha waimbaji mbalimbali wa nyimbo za Injili.

Msama alisema Profesa Mbarawa kukubali kuwa mgeni rasmi katika tamasha hilo ni ishara kwamba tamasha hilo halijaegemea upande mmoja wa dini kama inavyodhaniwa na baadhi ya wadau wa muziki huo.
“Tunampongeza Profesa Mbarawa kuwa mgeni rasmi katika Tamasha la Pasaka, kwani huwa halijali dini, jinsia wala kabila katika utekelezaji wake,” alisema Msama.

Msama alisema hivi sasa kamati yake ya maandalizi inaendelea na mchakato wa kufanikisha tamasha hilo ambalo litaanzia mkoani Geita Machi 26, Mwanza Machi 27 na kumalizia Kahama Machi 28.
Msama anataja viingilio katika tamasha hilo ni shilingi 5000 kwa wakubwa na shilingi 2000 kwa watoto ambako kupitia tamasha hilo amepanga kugawa baiskeli za walemavu 100 kwa wakazi wa mikoa hiyo na kwingineko.

Waimbaji waliothibitisha kushiriki tamasha hilo ni Rose Muhando, Upendo Nkone, Joshua Mlelwa, Jesica BM, Christopher Mwahangila, Christopher Mwabuka, Jenipher Mgendi, Bonny Mwaitege, Goodluck Gozbert, Kwaya za Wakorintho Wapili ya Mafinga na AIC Makongoro Vijana ya jijini Mwanza na wengineo wengi.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com