METDO Tanzania

METDO Tanzania

Wednesday, August 2, 2017

POLEPOLE: TUNAMPUUZA MBOWE

Katibu wa Halmashauri kuu ya taifa ya Ccm itikadi na uenezi Ndugu Humphrey Polepole amesema Ccm na serikali yake hawana mda wa kulumbana na Chadema kupitia mwenyekiti wake Mheshimiwa Freedman Mbowe kwani kazi yao kubwa kama chama tawala ni kuhakikisha kuwa wanatimiza ahadi walizoahidi kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 ambazo ni pamoja na kuwaletea wananchi maendeleo na kuinua uchumi wa nchi.

Polepole ameyasema hayo alipotakiwa kutoa ufafanuzi na mtandao wa darmpya.com juu ya kauli ya mwenyekiti wa Chadema Mheshimiwa Freeman Mbowe aliyoitoa jana jijini Dar es salaam juu ya serikali ya ccm chini ya Rais John Pombe Magufuli kushindwa kundesha nchi na kusababisha mtikisiko wa uchumi na hali ya maisha ya watanzania kwa ujumla kuendelea kuwa mbaya siku hadi siku.Mheshimiwa Mbowe aliitupia lawama serikali kwa kushindwa kusimamia uchumi na kusababisha hali mbaya kwa wananchi wa kipato cha chini huku ikiwabambikia kesi matajiri na wafanyabiashara wakubwa kwa kisingizio cha kukwepa kodi.

“Sisi tuna mkataba na wananchi kuhakikisha tunawaletea maendeleo,kwa sasa tuko busy kufanya kazi hiyo,hatuna mda wa kufanya malumbano yasiyokuwa na tija,tunajua tuna kazi kubwa mbele yetu ambayo tumesaini mkataba na wananchi mpaka mwaka 2020”.Hatuna mda wa kuhangaika na watu wasiokuwa na dhamira njema na nchi hii ambao wao kazi yao ni kupinga kila kinachofanywa na serikali,amesisitiza Polepole

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com