METDO Tanzania

METDO Tanzania

Saturday, August 5, 2017

Mhandisi Mtigumwe aipongeza MIVARF kwa kusaidia Wakulima nchini

Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi (KILIMO) Mhandisi Mathew Matigumwe amepongeza juhudu zinazofanywa na Mradi wa MIVARF ambao utatekelezwa na kuratibiwa na Ofisi wa Waziri Mkuu.

Mratibu wa Mradi huo kwa upande wa Mfumo wa Stakabadhi Ghalani, Bwana Julius Kallambo amemwambia Mhandisi Mtigumwe kuwa Mradi wa MIVARF umekuwa ukiwasaidia Wakulima wanaolima mazao ya kimkakati kama alizeti na mchele na kuongeza kuwa Mikoa ya Singida, Dodoma na Mbeya Wakulima wa maeneo hayo wamekuwa wakinufaika moja kwa moja na Mradi huo kwa kupatiwa mafunzo ya namna ya kuzalisha, kuhifadhi, kusindika na kutafuta masoko kwa kuongeza thamani (Value addition).

Mhandisi Mtigumwe amesema, juhudu zinazofanywa na Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu ni uthibitisho tosha kuwa Wadau wengi sasa wameanza kuitekeleza kwa vitendo thana ya ujenzi wa Viwanda vidogo na vya Kati kwa lengola kuzalisha malighafi ambazo zitatumika katika Viwanda vya ndani na baada ya hapo kuziuza katika soko la ndani ambalo hatujalitosheleza bado.

“Nawapongeza MIVARF kwa juhudi hizi ambazo, zinapaswa kuungwa mkono na Wadau wote na kwa namna ambayo mmewawezesha wakulima wa alizeti na mchele kulima na kuzalisha kwa tija na baada ya hapo wanazifungasha na kuuza kwa thamani ya juu, huu ni mfano mzuri wa kuigwa na kuendelezwa” Amekaririwa Mhandisi Mtigumwe.

Mhandisi Mtigumwe ameongeza kuwa, juhudi hizo za MIVARF zimesaidia na kuwafanya Wakulima kuanza kujitegemea kwa kufungua Kampuni zao binafsi mfano mmoja ni kuanzishwa kwa Kampuni ya USANGU Marketing Company LTD ambayo imekuwa ikinunua mchele kutoka kwa Wakulima wenzao kwa bei nzuri na kuuza mchele huohuo kwenye masoko makubwa ya Kitaifa na Kimataifa.

MWISHO
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com