METDO Tanzania

METDO Tanzania

Tuesday, April 28, 2020

WAZIRI HASUNGA AWAPA RUNGU WAKULIMA WA KAHAWA KUTAFUTA MASOKO NJE YA NCHI

Waziri wa Kilimo, Mhe Japhet Hasunga (Mb)
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma
WAKULIMA wa Zao la Kahawa nchini wametakiwa kuingia makubaliano na wanunuzi wa zao hilo kutoka nje ya nchi pindi wanapotoa bei nzuri ili wapate soko la moja kwa moja.
Kauli hiyo ilitolewa na Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga wakati akizungumzia mafanikio yaliyopatikana katika sekta ya Kahawa katika kipindi cha serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli.
Waziri huyo amebainisha kuwa Serikali itasimamia suala hilo kuhakikisha linatekelezeka kwa mujibu wa makubaliano ya wakulima na wanunuzi hao kutoka nje ya nchi.
“pale ambapo wakulima wanaweza kuingia makubaliano na wanunuzi kutoka nje na wanunuzi wakatoa bei nzuri ili wapate soko la moja kwa moja kufuatia makubaliano yalivyo kama serikali tutasimamia suala hilo kuhakikisha linatekelezeka” Alikaririwa Mhe Hasunga
Alibainisha kuwa sambamba na jitihada za kutafuta masoko nje ya nchi zipo nchi ambazo mpaka sasa zimekuwa ni wanunuzi wakubwa wa kahawa.
Alitaja nchi hizo kuwa ni pamoja na Ujerumani, Japani, Marekani, italia, Afrika Kusini na Morocco ambao wamekuwa wanunuzi wakubwa wa zao hilo.
“Lakini tunataka sasa tuongeze jitihada, masoko zaidi yatafutwe ili kuwa na masoko mengi zaidi, hatimaye tuweze kuongeza uzalishaji, ”alisisitiza Hasunga.
MWISHO
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com