Rais
wa Urusi, Vladimir Putin ameagiza kuondolewa wanadiplomasia na
wafanyakazi 755 wa Marekani waliopo nchini humo na anafikiria kuchukua
hatua za nyongeza kulipiza kisasi kwa vikwazo vya uchumi ilivyowekewa
nchini hiyo.
Putin
alisema jana katika mahojiano ya moja kwa moja kwenye televisheni ya
taifa kwamba aliagiza hatua hizo kwa sababu “alifikiri ulikuwa wakati wa
kuonyesha kwamba hawawezi kubaki bila kujibu mapigo."
Utekelezwaji
wa agizo la usitishwaji shughuli za wafanyakazi hao wa ubalozi wa
Marekani nchini Urusi unatarajiwa kuwa Septemba Mosi mwaka huu. Watabaki
wafanyakazi 455.
Desemba
2016, aliyekuwa rais wa Marekani, Barack Obama aliamuru kutimuliwa
wanadiplomaisa 35 wa Urusi kutokana na tuhuma za Urusi kuingilia
uchaguzi wa Marekani kupitia njia ya mtandao.
Jumanne
iliyopita mabunge yote mawili ya Congress ya Marekani yaliidhinisha kwa
wingi wa kura vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Urusi.
Mashirika
ya ujasusi nchini Marekani yanaamini kuwa Urusi ilijaribu kuingilia
uchaguzi wa urais wa mwaka 2016 kwa lengo la kumsaidia Donald Trump
kupata ushindi.
Urusi imekuwa ikikanusha kuingilia kwa vyovyote uchaguzi huo.
Urusi imekuwa ikikanusha kuingilia kwa vyovyote uchaguzi huo.
0 comments:
Post a Comment