Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu leo July 31, 2017 imetoa siku saba kwa upande wa
mashtaka ufanye jitihada za kukamilisha upelelezi wa kesi inayowakabili
Rais wa Simba SC, Evans Aveva na Makamu wake Geofrey Nyange ‘Kaburu’.
Hatua
hiyo imekuja baada ya Mwendesha Mashitaka wa TAKUKURU, Leonard Swai
kudai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Victoria Nongwa kuwa upelelezi wa
shauri hilo haujakamilika.
Upande
wa utetezi ukiongozwa na Wakili Mtakyamirwa Philemon ulidai mara ya nne
sasa upande wa mashitaka unadai upelelezi haujakamilika na kudai
wanatakiwa kuhakikisha wanakuwa makini na shauri hilo ili wakamilishe
upelelezi kwani washitakiwa wako ndani kwa kosa lisilo na dhamana.
Hata hivyo, Swai alidai kuwa mashitaka ya kughushi wanahitaji upelelezi wa kina hivyo anaomba Mahakama kuwapa siku 14.
Hakimu
Nongwa alisema Mahakama imezingatia hoja za pande zote mbili kwamba
mashitaka ya kughushi yanachukua muda mrefu kukamilika na kusisitiza
kuwa licha ya sheria kutaka kuahirishwa kwa kesi kusizidi siku 14 ombi
la upande wa utetezi lina maana hivyo kutoa muda huo ili kama
washitakiwa wana kosa watiwe hatiani.
Hakimu Nongwa aliahirisha kesi hiyo hadi August 7, 2017 kwa ajili ya kutajwa.
0 comments:
Post a Comment