METDO Tanzania

METDO Tanzania

Thursday, July 20, 2017

MD KAYOMBO AKABIDHI MIPIRA MINNE KWA AJILI YA MASHINDANO YA MALONGO CUP 2017 KIJIJINI KWAO MISASI

Na Mathias Canal, Misasi-Mwanza

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es salaam Ndg John Lipesi Kayombo akiwa mapumzikoni Kijijini kwao Misasi, Kata ya Misasi, Wilaya ya Misungwi, Mkoani Mwanza leo 20 Julai, 2017 Amekabidhi mipira minne kwa viongozi wa Mashindano ya mpira wa Miguu kwa wanaume yajulikanayo kama MALONGO CUP 2017.

Makabidhiano ya Mipira hiyo yamefanyika katika uwanja wa CCM-Misasi kabla ya kuanza kwa mchezo wa Hatua ya pili ya MASHINDANO hayo yaliyoanza kurindima hapo Jana katika Viwanja vya CCM-Misasi ambapo yanataraji kufika ukomo siku ya Ijumaa Agosti 18, 2017 huku yakitarajiwa kuwa yamewafikia vijana zaidi ya 500 katika Kijiji cha Misasi na vijiji vingine vya jirani.

Pamoja na mipira hiyo minne aliyoikabidhi Mkurugenzi Kayombo kwa mdhamini wa Mashindano hayo ambaye ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Misasi Ndg Malongo Magese pia amemkabidhi Pampu ya kisasa kwa ajili ya kutumika kujaza upepo katika mipira hiyo pindi upepo unapopungua.

Akizungumza Mara baqda ya kukabidhi mipira hiyo Mkurugenzi Kayombo aliwakumbusha washiriki wote wa Mashindano hayo kutambua kuwa wanapaswa kufahamu kuwa Michezo inaimarisha Afya, Amani, Umoja na Mshikamano hivyo Mashindano hayo yatakuwa chachu pia katika kuimarisha Undugu na kupunguza matendo ya uhalifu.

Alisema kuwa ameamua kukabidhi mipira hiyo kutokana na kuona Mashindano hayo yakiendelea pasina kuwa yamekamilika kwa kuwa na vitendea kazi kama vile mipira na Jezi kwa ajili ya wachezaji.

Alisema kuwa Vijana wanapaswa kutumia nguvu walizonazo kwa kufanya kazi kwani wao ndio nguvu kazi ya Taifa huku akiwasihi kutojihusisha na matendo maovu ya matumizi ya Dawa za kulevya.

Aidha, Lengo la mashindano hayo ni kuinua vipaji kwa vijana, Kuimarisha mahusiano chanya kwa Vijana sambamba na kuhamasisha Vijana kufanya kazi kwa bidii na kuachana na dhana ya kushinda vijiweni pasina kazi za kufanya.

MASHINDANO hayo yanashirikisha timu 13 ambazo ni Timu ya Misasi Starz A Fc, Wega Fc, Inonelwa Fc, Mchongomani Fc, na Manawa Fc

Zingine ni Timu ya Misasi Starz B Fc, Kijama Fc, Nyashimba Fc, Ikungumhula Fc, Mwashilungi Fc, Igobeko Fc, Mwasagela Fc, na Iseni Fc.

Sambamba na hayo pia Mkurugenzi Kayombo ameahidi kutoa shilingi laki moja moja kwa timu zitakazoshika nafasi za juu hususani timu itakayokuwa bingwa, mshindi wa Pili, wa Tatu na Mshindi wa nne. Pia ametoa mipira mitatu kwa ajili ya kutumika katika mashindano hayo.

MASHINDANO ya MALONGO CUP 2017 yanadhaminiwa na Mwenyekiti wa Kijiji cha Misasi Ndg Malongo Magese.

Kwa upande wa baadhi ya wachezaji hao wakizungumzia msaada huo waliopatiwa, wamempongeza Mkurugenzi Kayombo kwa jambo hilo na kuahidi kujifunza mipira hiyo ili iweze kuwasaidia katika Mashindano hayo sambamba na Mashindano mengine mbalimbali.Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es salaam Ndg John Lipesi Kayombo akikabidhi mipira kwa ajili ya Mashindano ya Malongo CUP 2017 yanayofanyika Kijijini kwao Misasi, Kata ya Misasi, Wilaya ya Misungwi, Mkoani Mwanza.Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es salaam Ndg John Lipesi Kayombo akikabidhi mipira kwa ajili ya Mashindano ya Malongo CUP 2017 yanayofanyika Kijijini kwao Misasi, Kata ya Misasi, Wilaya ya Misungwi, Mkoani MwanzaBaadhi ya wananchi wakifatilia dhifa ya kukabidhi mipira iliyofanywa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es salaam Ndg John Lipesi Kayombo kwa ajili ya Mashindano ya Malongo CUP 2017 yanayofanyika Kijijini kwao Misasi, Kata ya Misasi, Wilaya ya Misungwi, Mkoani MwanzaBaadhi ya wadau wa michezo wakiongozwa na Flora Magabe kushiriki dhifa ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es salaam Ndg John Lipesi Kayombo akikabidhi mipira kwa ajili ya Mashindano ya Malongo CUP 2017 yanayofanyika Kijijini kwao Misasi, Kata ya Misasi, Wilaya ya Misungwi, Mkoani MwanzaMkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es salaam Ndg John Lipesi Kayombo akiongozana na wadau wengine wa michezo kwa ajili ya kukabidhi mipira itakayotumika kwenye Mashindano ya Malongo CUP 2017 yanayofanyika Kijijini kwao Misasi, Kata ya Misasi, Wilaya ya Misungwi, Mkoani Mwanza.Baadhi ya wananchi wakifatilia moja ya mechi kati ya Misasi Starz B Fc na Kijima Fc inayofanyika Kijiji cha Misasi, Kata ya Misasi, Wilaya ya Misungwi, Mkoani MwanzaMkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es salaam Ndg John Lipesi Kayombo akikabidhi mipira kwa ajili ya Mashindano ya Malongo CUP 2017 yanayofanyika Kijijini kwao Misasi, Kata ya Misasi, Wilaya ya Misungwi, Mkoani MwanzaMkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es salaam Ndg John Lipesi Kayombo akikabidhi mipira kwa ajili ya Mashindano ya Malongo CUP 2017 yanayofanyika Kijijini kwao Misasi, Kata ya Misasi, Wilaya ya Misungwi, Mkoani Mwanza

Share:

1 comment:

  1. Jambo jema sana ulilolifanya katika jamii ya kijiji chetu tunaona uwajibikaji wako katika jamii ya kijiji chetu cha misasi nasi tumepokea kwa furaha kubwa sana katika mapumiko haya na hamasa kubwa uliyoifanya katika vijana wenzetu na jamii nzima katika kijiji chetu

    ReplyDelete

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com