METDO Tanzania

METDO Tanzania

Wednesday, September 6, 2017

WANACHAMA WATATU WA CUF WAFA AJALINI PWANI.

Watu watatu wamefariki dunia na wengine watatu kujeruhiwa baada ya gari aina ya Toyota Noah kugongana na lori eneo la Ubena Zomozi mkoani Pwani usiku wa kuamkia leo.
Naibu mkurugenzi wa ulinzi na usalama wa CUF, Masoud Mhina akizungumzia ajali hiyo, amesema waliokufa ni wanachama wa chama hicho mkoani Tanga.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Onesmo Lyanga amesema ajali hiyo ilitokea saa 8:30 usiku wa kuamkia leo Septemba 6 baada ya Toyota Noah lililokuwa likitokea Dodoma kuhama njia na kugongana na lori.
Lyanga amesema lori hilo lilikuwa likiendeshwa na Yassin Hamad mkazi wa Dar es Salaam.
Amesema waliokufa katika ajali hiyo ni Uledi Salumaa (32) ambaye alikuwa dereva wa Toyota Noah, Mary Komba (40) na mwingine aliyetambuliwa kwa jina moja la Isack, wote wakazi wa Muheza mkoani  Tanga.
Kamanda Lyanga amewataja majeruhi wa ajali hiyo kuwa ni Juma Nindi, Chausiku Hassan na Esther Masie ambao pia ni wakazi wa Muheza.

By Muyonga Jumanne, MCL.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com