Wadau
wa zao la pamba mkoani Simiyu wamekutana na kufanya kikao lengo likiwa ni kujadili
masuala mbalimbali yanayohusu mstakabali wa zao hilo kuelekea katika kipindi
cha msimu wa kilimo kwa mwaka 2017/2018.
Kikao
hicho kimewahusisha Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, Wakuu wa Wilaya, Makatibu
Tawala wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, Wenyeviti wa Halmashauri, Maafisa
Kilimo, Wamiliki na wataalam wa Makampuni ya Ununuzi wa Pamba kutoka ndani ya
nje ya Mkoa wa Simiyu ambacho kiliongozwa na Mkuu wa Mkoa huo, Mhe.Anthony
Mtaka.
Akifungua
kikao hicho Mkuu wa Mkoa wa Simiyu amesema Mkoa huo unazalisha zaidi ya
asilimia 55 ya pamba yote hapa nchini, hivyo akawataka wadau wa pamba mkoani
humo kutumia vema kikao hicho kujadili kwa umakini masuala muhimu katika sekta
ya pamba ili wananchi waweze kuzalisha kwa tija na kunufaika na zao hilo.
Katika kikao hicho Wadau wa zao la pamba wamekubaliana kuwa kilimo cha mkataba kwa wakulima
kiwe cha hiari sio lazima na elimu indelee kutolewa kwa wakulima na wanunuzi wa
pamba kuona namna wanavyoweza kutumia kilimo cha mkataba kuongeza tija katika
uzalishaji kwa wakulima watakao kuwa tayari.
Akichangia
hoja katika kikao hicho Afisa Kilimo Halmashauri ya Wilaya Bariadi, Martha
Zongo, amesema kilimo mkataba kikifanyika kwa makubaliano yatakayowekwa baina
ya wakulima walio tayari na makampuni
yanayonunua pamba, wakulima wasio na uwezo watapata pembejeo na huduma za ugani
kutoka kwa wataalam wa Makampuni hayo na kuongeza uzalishaji maana katika
baadhi ya maeneo kuna upungufu wa maafisa Ugani.
Kuhusu suala la matumizi ya mbegu wadau walikubaliana
kuwa wananchi wa Mkoa wa Simiyu watapata mbegu zenye manyoya na zisizo na manyoya
kama ilivyoelezwa na Bodi ya Pamba na ni hiari yao kuchagua mbegu watakayoitaka,
hivyo elimu iendelee kutolewa kwa wakulima juu ya matumizi ya mbegu hizo ili waelewe
mbegu iliyo bora zaidi kwa uzalishaji wenye tija.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya
Meatu, Fabian Manoza amependekeza Taasisi ya Ukaguzi na Uthibitisho wa Mbegu
Nchini(TOSCI) waone umuhimu wa kufungua tawi Kanda ya Ziwa ili kufuatilia kwa
ukaribu udhibiti wa mbegu za pamba na Wakala wa Mbegu (ASA) watafute mashamba pia
katikakanda hii ili waweze kuzalisha mbegu kwa lengo la kurahisisha upatikanaji
wa mbegu bora za pamba.
Vile vile katika suala la mbegu Bw. Stephen Lawrence
kutoka Kampuni ya Nyanza Cotton inayojishughulisha
na ununuzi wa Pamba akiungwa mkono na wadau wengine, aliomba Serikali itoe
ruzuku kwa wakulima ili waweze kumudu gharama za ununuzi wa mbegu.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu aliwahakikishia wajumbe kuwa
mapendekezo na maazimio yaliyotolewa katika kikao hicho atayawasilisha katika
Kikao cha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Kasim Majaliwa na
Wakuu wa Mikoa inayolima pamba hapa nchini kitakachofanyika Mjini Dodoma,
tarehe 08/09/2017.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe.Anthony Mtaka(katikati) akizungumza na wadau wa zao la pamba Mkoani humo(hawapo
pichani) katika kikao kilichofanyika Mjini Bariadi ili kujadili suala la Kilimo
cha Pamba mkoani hapo(kushoto) Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe.Festo Kiswaga na
(kulia) Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe.Dkt.Titus Kamani.
Baadhi ya wadau wa zao
la pambaMkoani Simiyu wakifuatilia hoja mbalimbali zilizokuwa zikijadiliwa
katika kikao kilichofanyika Mjini Bariadi ili kujadili suala la Kilimo cha
Pamba mkoani hapo.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa
Simiyu, Mhe.Dkt.Titus Kamani akichangia hoja katika kikao cha Wadau wa pamba
Mkoani humo kilichofanyika Mjini Bariadi lengo likiwa ni kujadili mstakabali wa
zao hilo mkoani humo.
Bi.Suzan Mollel kutoka
katika Kampuni ya OLAM inayojishughulisha na ununuzi wa pamba iliyoko wilayani
Bunda, akichangia hoja katika kikao cha Wadau wa pamba Mkoani humo
kilichofanyika Mjini Bariadi lengo likiwa ni kujadili mstakabali wa zao hilo
mkoani humo.
Mbunge wa Jimbo la
Bariadi na Mmiliki wa Kiwanda cha pamba(Ginner), Mhe.Njalu Silanga akichangia
hoja katika kikao cha Wadau wa pamba
Mkoani humo kilichofanyika Mjini Bariadi lengo likiwa ni kujadili mstakabali wa
zao hilo mkoani humo.
Mkuu wa Wilaya ya
Meatu, Mhe.Dkt. Joseph Chilongani akichangia hoja katika kikao cha Wadau wa
pamba Mkoani Simiyu kilichofanyika Mjini Bariadi lengo likiwa ni kujadili
mstakabali wa zao hilo mkoani humo.
Ndg.Sebastiani Max
kutoka SHIRECU akichangia hoja katika kikao cha Wadau wa pamba Mkoani Simiyu
kilichofanyika Mjini Bariadi lengo likiwa ni kujadili mstakabali wa zao la
pamba mkoani humo.
Mkuu wa Wilaya ya
Busega, Mhe.Tano Mwera akichangia hoja katika kikao cha Wadau wa pamba Mkoani
Simiyu kilichofanyika Mjini Bariadi lengo likiwa ni kujadili mstakabali wa zao
hilo mkoani humo.
Mkurugenzi Mtedaji wa
Kampuni ya BioRe Tanzania inayojishughulisha na uzalishaji wa pamba hai(organic
cotton)Ndg. Niranjan Pattni, akichangia hoja katika kikao cha Wadau wa pamba
Mkoani Simiyu kilichofanyika Mjini Bariadi lengo likiwa ni kujadili mstakabali
wa zao hilo mkoani humo.
Ndg. Stephen Lawrent
(mwenye miwani) kutoka Kampuni ya inayojihusisha na Ununuzi wa Pamba ya Nyanza
Cotton akichangia hoja katika kikao cha Wadau wa pamba Mkoani Simiyu
kilichofanyika Mjini Bariadi lengo likiwa ni kujadili mstakabali wa zao hilo
mkoani humo.
Mwenyekiti wa
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa, Mhe.Lucas Hinda Mwaniyuki akichangia hoja
katika kikao cha Wadau wa pamba Mkoani Simiyu kilichofanyika Mjini Bariadi
lengo likiwa ni kujadili mstakabali wa zao hilo mkoani humo.
Afisa Kilimo wa
Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi, Martha Zongo akichangia hoja katika kikao cha
Wadau wa pamba Mkoani Simiyu kilichofanyika Mjini Bariadi lengo likiwa ni
kujadili mstakabali wa zao hilo mkoani humo.
Mkuu wa Wilaya ya
Itilima, Mhe.Benson Kilangi akichangia hoja katika kikao cha Wadau wa pamba
Mkoani Simiyu kilichofanyika Mjini Bariadi lengo likiwa ni kujadili mstakabali
wa zao hilo mkoani humo.
.Baadhi ya Wajumbe wa
Kamti ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu,
Mhe.Dkt. Titus Kamani wakifuatilia hoja mbalimbali zilizokuwa zikijadiliwa
katika kikao kilichofanyika Mjini Bariadi ili kujadili suala la Kilimo cha
Pamba mkoani hapo.
Katibu Tawala wa Wilaya
ya Maswa akichangia hoja katika kikao cha Wadau wa pamba Mkoani Simiyu
kilichofanyika Mjini Bariadi lengo likiwa ni kujadili mstakabali wa zao hilo
mkoani humo.
Ndg.Jeremia Malongo
kutoka Kampuni ya VITRESS inayojishughulisha na ununuzi wa pamba Mkoani Simiyu
akichangia hoja katika kikao cha Wadau wa pamba kilichofanyika Mjini Bariadi
lengo likiwa ni kujadili mstakabali wa zao hilo mkoani humo.
|
0 comments:
Post a Comment